TESTIMONIES


UTANGULIZI

Nimezaliwa na kuishi Namibia maisha yangu yote. Niliokoka tarehe 06/02/2005. Bwana Yesu amenifunulia mambo mengi ya ulimwengu wa roho pamoja na kunipeleka mara kadhaa kuzimu. Bwana  aliniambia  niwaelezee  watu  niliyoyaona;  na  akanionya  nisiongeze  wala  kupunguza chochote kwa yale aliyonionyesha au kuniambia. Kufikia kuandika kitabu hiki, mwisho wa 2006, nilikuwa nimetembelewa   na Bwana Yesu mara 33. Kwa kila utembezi huo Bwana alinisisitizia: MUDA UMEISHA.

SAFARI YA KWANZA KWENDA KUZIMU
Mwisho wa juma la 23/07/2005, nilichukua teksi kutoka mji wa Ondangwa (Nchini Namibia)
ninakoishi na kufanya kazi, kuelekea kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu. Nilipokwa njiani nilihisi kuwa kitu cha ajabu kilikuwa kinaenda kutokea jioni hiyo. Nilifika nyumbani mwendo wa saa kumi na mbili jioni na ndio wakati watu walikuwa wakiandaa chakula cha jioni. Nilikuwa jikoni na ndugu zangu nimelala juu ya shuka kukuu  chini, na wapwa zangu walikuwa wakiimba nyimbo za kanisani.

Ghafla nikahisi nguvu kuu za Mungu juu yangu zilizoufanya mwili wangu kuzimia. Nilimwona mtu mwenye kanzu nyeupe na kamba yenye rangi sawa, akinisogelea nilipokuwa nimelala. Kulikuwa na mwanga wa ajabu unamzunguka kana kwamba unatoka kwake. Alikuwa amevaa viatu vya hudhurungi. Alifanana na watu wa mashariki ya kati hata ngozi ikawa inampenda. Mwili wake ulikuwa umejaa utukufu nilishindwa kumwangalia kwenye macho. Alipoongea sauti yake ilikuwa ya upole, huruma, upendo, na yenye mamlaka. Mawimbi ya upendo yalikuwa yakinijia kutoka kwake.

Akainyosha mikono yake kuelekea kwangu na kuniinua. Ghafla nikajikuta nipo katika mwili mzuri uliobadilishwa. Nilionekana kama vile nilivyo kuwa kijana wa miaka kumi na nane. nilikuwa nimevalia kanzu nyeupe iliyofungwa kamba nyeupe. Ijapokuwa kanzu yangu ilikuwa nyeupe lakini malighafi yake  ilikuwa tofauti na kanzu yake. Vazi lake lilikuwa la kitani safi na mwanga na mng’ao wake ni vigumu kuelezea.

Alisema kwa upendo na sauti ya upole, ’Victoria fuatana   nami, nitakuonyesha mambo ya kuogopesha na kukupeleka sehemu ambayo hujawahi kuona maisha yako yote.
Akanishika mkono wa kuume na tukaanza kuenda. Nilihisi kama vile tunatembea hewani na tunapand wakati   wote.   Baad ya   mud njiani   nikawa   nimechoka   sana.   Nikamwambia nisingeweza kuendelea na safari na nikaomba kurudi nyumbani.

Aliniangalia kwa upole na kusema Haujachoka uko safi, ukichoka nitakubeba. Lakini sasa uko safi. Amani na iwe nawe, tuondoke”.
Sehemu tuliyofika ilikuwa kame na mbaya kuliko jangwa lolote baya lililojulikana na binadamu, bila dalili yoyote ya uhai au maisha. Hapakuwa na mti wowote, nyasi au kiumbe chenye uhai hakikuonekana. Ilikuwa ni sehemu mbaya sana.
Tulikuja kwenye lango na yule mtu akanigeukia akisema, Victoria tutapitia langoni na vitu utakavyofundishwa vitakuogopesha na kukufadhaisha. Lakini uwe na uhakika kokote nitakako kupeleka utalindwa vizuri. Fungua macho yako uangalie kila kitu nitakacho kuonyesha”. Nilitishika na kuanza kulia. Nilipinga na kutaka anirudishe.
Nikamwambia kuwa sikutaka kuingia mahali pale kwakuwa nilikuwa naona yanayotendeka ndani akaniambia, Amani na iwe nawe; niko pamoja nawe ni lazima tuingie ndani, kwa maana MUDA UMEISHA.



Kuzimu kulivyo
Tukapita lango lile mpaka ndani na kwa niliyoyaona nashindwa kusimulia mahali pale palivyo.
Ninuhakika  hakunmahali  pengine  dunianpa  kutisha  kampale.  Mahali  pale  palikuwa pakubwa sana na nilihisi kuwa palikuwa panaongezeka  wakati wote. Giza la mahali pale lilikuwa kubwa  sana  na  moto  uliokuwa  unawaka  haupimiki.  Moto  wenyewe  au  miali  yake  ilikuwa


haionekani ila ukali wake ulikuwa juu sana. Nzi wa kila namna na rangi walikuwa kila mahali. Palikuwepo pia na minyoo wafupi, wanene na weusi wakijaribu kupanda juu ya kila kitu. Minyoo wakanza kupanda juu yetu huku inzi wakiruka kila mahali. Harufu ya mahali pale ilikuwa mbaya mno, ilikuwa kama  nyama iliyooza ila ni zaidi ya mara mia ya harufu yoyote ile niliyo wahikuihisi. Kulikuwa kumejaa sautu za vilio na kusaga meno, pia nilisikia vicheko viovu vya pepo wabaya.

Cha kuhuzunisha ni kuwa mahali pale palikuwa pamejaa watu wasiohesabika.   Watu walikuwa kwa namna ya mifupa. Nilijua mifupa hiyo ilikuwa ni watu kwani niliweza kwa uhakika kuwajua ndugu zangu kutoka kijijini kwetu. Mifupa hiyo ya rangi ya kijivu ilikuwa imekauka sana. Walikuwa na meno makali  kama ya wanyama,  midomo mikubwa na ndimi ndefu na nyekundu. Mikono na miguu ilikuwa na vidole virefu vyenye kucha za kutisha. Wengine walikuwa na mikia na pembe.

Pepo wachafu walikuwa wakichangamana na watu. Mapepo hao walikuwa kama kenge wakitembea kwa miguu minne. Waliifurahia hali ile na wakawa wakiwatesa na kuwakejeli wanadamu, huku wao wakirukaruka na kushangilia wakati wote. Wanadamu kwa upande wao walionekana wa kusikitisha na kuvunjika moyo, walionekana kukata tamaa na bila matumaini yoyote. Kelele za wanadamu zilikuwa kwasababu ya maumivu. Walikuwa wakilia, kupaza sauti na kusaga meno. Hali yao haikuwa ya kusikitisha tu, bali pia ya uchungu na masitikiko.Watu wa mahali pale walikuwa wengi lakini niliona wazi kuwa wengi walikuwa wanawake.

Makundi ya watu kuzimu
Waligawanywa kwa makundi tofauti lakini haikuwezekana kuwahesabu kwa makundi yao kwani
walikuwa wengi sana. Niliyekuwa naye akanipeleka kwa kikundi kimoja cha mashariki na kuniambia, Hili ni kundi la walioshindwa KUSAMEHE. Niliwaeleza mara nyingi na kwa njia tofauti jinsi ya kuwasamehe wenzao lakini wao wakakataa. Niliwasamehe dhambi zao zote lakini wao wakakataa kuwasamehe wengine. Muda wao duniani ulipoisha wakajipata mahali hapa. Watakuwa  mahali  milele yote,  wanavuna  matunda  ya  matendo  yao  milele na  milele.  Ila  ni uchungu kwangu kuwaona hapa katika hali hii kwa kuwa nawapenda.

Nikaongozwa  kwa  kundi  la  pili  na  nikaambiwa  nyule  mwenye  kunipeleka,  kuwa  walikuwa wenye MADENI na makundi yao yalikuwa matatu:

1 Wa kwanza ni wale waliodaiwa na wenzao na walikuwa na uwezo wa kulipa lakini wakawa wakihairisha siku baada ya siku. Wangeahidi kulipa wakati ujao, mwezi ujao, mwaka ujao mpaka muda wao duniani ukaisha na wakajipata mahali hapa. Watakaa mahali hapa milele na milele wanavuna matunda ya kazi yao.

2 Wa  pili  ni  wale  waliodaiwa  madeni  waliyoweza  kulipa  na  walikuwa  tayari  kulipa  lakini waliogopa madhara yake. Waliona kuwa wakiongea ukweli watakataliwa, watapelekwa jela au walichokifanya kingejulikana dunia yote na wangedhalilishwa. Yule mtu akaniambia, Hakuna  hata  mmoja  aliyeniuliza  njia  ya  kulipa.  Wangefanya  hivyo  ningewaonyesha  njia rahisi. Walitumia hekima na sababu zao ambazo hazikuwasaidia hata kidogo”.

3.   Waliokuwa  na  madeni  wasiyoweza  kulipa  ila  hawakuniambia  kwamba  wana  madeni wasiyoweza kulipa. Wangefanya hivyo ningewalipia madeni yao. Pia walijaribu kutumia hekima na sababu zao, ambazo hazikuwasaidia hata kidogo. Sasa wamejikuta sehemu hii wasiyoweza kutoka. Wanakula matunda ya matendo yao. Moyo waniuma kwa ajili ya hawa wote kwasababu nawapenda sana.

Katika kundi la kwanza niliwaona ndugu zangu wawili wa kike wa karibu, vilevile na ndugu yangu mmoja wa miaka kumi na miwili. Nilijua miaka yake kwani huo ndio uliokuwa umri wake alipofariki. Katika kundi la pili niliwaona baadhi ya ndugu zangu na hata mchungaji niliyekuwa namfahamu vizuri. Jakes mpenzi wangu aliyejinyonga baada ya mimi kuokoka  alikuwa kwenye kundi la pili. Niliwaona baadhi ya majirani zangu katika makundi yote.

Niliwajua  watu  tuliokuwa  tukifahaminiana  na  wao  pia  wakanijua.  Watu  wa  ukoo  wetu waliponiona  walianza  kunitukana  kwa  lugha  chafu.  Mmoja  wao  akaniambia  kuwa  sikustahili


kumfuata yule niliye kuwa naye. Wakanikumbusha hali niliyokuwa kabla ya wokovu. Waliyoyasema yalikuwa kweli kwani ni mambo niliyoyafanya. Jakes mpenzi wangu akasema kuwa nilikuwa wake na nilistahili kuwa alipokuwa maana dhambi zetu zilikuwa sawa. Mwanzoni Mchungaji   alifurahia   kunion nikiend alikokuwa,   lakin alipoona   niliyeandaman naye akaungana na wenzie kunitukana. Aliyekuwa nami akaniambia niyapuuzie maneno hayo kwani hawakujua walichokuwa wakifanya.

Nikaogopa na kushikwa na huzuni sana, nilikuwa nikitetemeka nikashindwa kusimama. Nikalia bila kujizuia ndipo niliyekuwa naye akanikumbatia na kusema, Amani na iwe nawe Victoria. Palepale nguvu zikanirudia na nikapata faraja na amani kuwa naye. Wakati wa kuondoka ukawa umefika  naye  akasema, Victoria nimekuonyesha  haya  ili uchaguni  kundi  lipi ungependa kuwa, kwa kuwa uamuzi ni wako. Lazima uwaambie watu kila kitu ulichoona bila kupunguza au kuongeza kitu chochote.”



Kurudi kutoka kuzimu
Nakumbuka tulipotoka mahali pale pa mateso tukiwa pamoja, ila sijui nilipomuacha kwasababu
niliposhtuka na kufungua macho nilijikuta mwilini kama kawaida. Nilikuwa nimelazwa hospitali ya Oshakati. Kulikuwa na mpira wa kuingizia maji mwilini, mamangu na ndugu zangu walikuwa chumbani humo. Machozi yalikuwa hayajamkauka mamangu. Nilipomuuliza Nesi kilichokuwa kikiendelea akaniambia, Umerudishwa, pengine una makosa na unahitaji kutubu.”
Japo  Nesi  aliongea  kwa  furaha  bado  niliona  anaogopa  kunisogelea.  Nikamuulizia  daktari aliyekuwa akinishughulikia.

Daktari  alipofka  hakuweza  kuelezea  ugonjwa  niliokuwa  nao.  Alidhania  kuwa  malaria  lakini matokeo hayakuonyesha hivyo. Joto la mwili na shinikizo la damu vyote vilikuwa chini sana lakini hakujua sababu yake. Hakujua la kufanya kwani hangeweza kunilaza Hospitalini kwani sikuwa mgonjwa. Maji waliyoniingizia kwa mpira yalikuwa hayaingii vizuri lakini mara tu nilipofungua macho yakaanza kuingia bila tatizo. Daktari akaagizia niongezewe maji mengine.

Niliendelea  kuhofu  na  kulia  kwa  ajili  ya  mahali  pale  pa  mateso.  Matukio  ya  mahali  pale yaliendelea kupita machoni kwangu saa zote. Sikuweza kulala mwili mzima ulikuwa unaumwa, viungo vyote vilikuwa kama vimetenganishwa na kuunganishwa tena. Tumbo lilinisumbua na kichwa kikaniuma juma zima.

Niliamua kutomwelezea mtu yeyote niliyoyaona. Ni nani atakayeniamini? Watu wangenichukuliaje? Nikajiwazia. Baada ya siku tatu nikamwambia mama mmoja aniombee na nikaishia kumwelezea yote yaliyotokea. Nikajihuzunikia sana kwa kuisimulia hadithi hiyo maana sasa haingeweza kufichika. Mwishowe nilielewa kuwa Mungu ni Mungu. Akitaka kitu kisimuliwe sina uwezo wa kukizuia eti kwasababu ya ya mawazo na hofu yangu.

Maelezo juu ya safari
Agosti 19, niliamka nikihisi nguvu za Mungu. Nilikuwa dhaifu nikitetemeka na nikajisikia kama
nguvu za umeme zinapita mwilini. Jioni nikaona miale ya mwanga mkuu na katikati yake nikamwona mtu yule aliyenipeleka sehemu ya mateso. Wakati huu akaketi kwenye kiti karibu na kitanda changu. Kiti chenyewe hakikuwepo lakini alipotaka kukaa kilionekana. Kilikuwa kiti cha mapambo mazuri huku kikiwa kimeundwa na dhahabu tupu.

Baada  ya  kunisalimia  akaniambia  kuwa  anaelewa kuwa  ninmaswali  mengi  na  ndio  maana alikuwa  amejitokeza  ili  ajieleze  yeye  na  mambo  mengine  yaliyokuwa  yametokea.  Akaanza kusema,
Mimi ni Yesu, mwokozi wako, kama una mashaka yoyote angalia mikono yangu. Mahali
tulikokwenda ni  kuzimu. Nikaona mahali alipogongwa misumari.

Rafiki ningependa nikwambie kuwa kuzimu sio mawazo ya mtu bali ni mahali pabaya pa mateso kulikotengenezewa shetani na mapepo yake. Wanadamu wanastahili kwenda mbinguni pamoja


na Yesu lakini lazima tumchague yeye kabla hatujachelewa. Leo ukisikia sauti yake usiufanye moyo  wako  kuwa  mgumu.  Mkubali  Yesu  kama  mwokozi  wako,  na  kama  umempokea  basi mwishie yeye.

Sikujua sababu ya kuambiwa nichague kati ya makundi mawili huko kuzimu na ilhali mimi nimeokoka. Nimemwamini yeye na bado ananiambia nichague kwenda kuzimu au la. Sikumuelewa. Nikamwomba Mungu anifunulie maana ya usemi huu na kile angetaka nifanye. Akaniambia kuwa nilikuwa mtu wa HASIRA na pia SIKUWASAMEHE dadangu na binamu yangu mmoja. Nikaomba msamaha kwa dhambi hiyo  halafu nikamwomba dada msamaha kwa kuweka hasira na chuki dhidi yake. Ikabakia kwenda kumwomba binamu msamaha.

Bwana akanikumbusha kuwa niliwahi kupata ajira ya ualimu nikitumia cheti bandia cha diploma. Akasema kuwa kitendo hicho ni DENI pamoja na WIZI. Nilitaka kutenda lililo haki na nikamwomba anipe njia nzuri ya kufuata kwani hilo lilitosha kunipeleka gerezani. Akaniambia nikatubu kwenye idara ya elimu. Nilikuwa tayari kwa lolote, hata kwenda gerezani ikiwa haiwezi kuepukika. Mungu akatenda maajabu na wakuu wakaniambia nichague kama nataka kulipa au la. Hawakutaka kunipeleka mahakamani kwasababu kukiri kwangu kuliwashangaza. Hakika Mungu ni wa ajabu na analiheshimu neno lake.

Ukiwa na jambo kama hili nakusihi kufanya kilicho cha haki bila kujali matokeo. Unaweza ukafungwa jela hapa dunuiani lakini hiyo ni ya muda. Hakuna uchungu au fedheha inayoweza kufananishwa na kutengwa na Mungu milele na milele. Kuzimu sio mahali pazuri; ni afadhali umwache Mungu akuhukumu sasa kabla haujachelewa. Tusiogope hukumu ya Mungu katika siku hizi za neema, NI VYEMA TUMWACHE YEYE ADHIHIRISHE CHOCHOTE KILICHO KIBAYA MAISHANI MWETU KAMA BADO TUNA WAKATI WA KUJIREKEBISHA kwani hakuna msamaha upande ule mwingine wa kaburi.



SAFARI YA PILI KUZIMU
Tarehe 18/10/2005, niliamka saa kumi na moja unusu alfajiri, sikuweza kwenda kazini. Nilikuwa
najisikia dhaifu sana na nikawa nimenyongonyea; nisingeweza kujisogeza au kugeuka kitandani
pangu, uwepo wa Mungu ulikuwa mkubwa chumbani. Nilikuwa nikitetemeka na kuhisi kama nguvu  za  umeme  zinapita  mwilinmwangu.  Bwana  akaja  kunichukua  kabla  ya  saa  mbili. Alinisalimu na kuniambia kuwa inatupasa kwenda tena kwani MUDA UMEISHA. Nikasimama na tukaanza kutembea. Jinsi tulivyokuwa tukitembea siku hii ilikuwa tofauti na siku zingine. Japo miguu yetu ilikuwa ikitembea, ilikuwa ni kama tunaogelea zaidi kuliko kutembea.
Tukiwa safarani, Yesu akaniambia, Dhambi zote ni mbaya na hakuna dhambi kubwa wala ndogo Dhamb zote   huleta   mauti haijalish ukubw wal udogo Akaniambia   kuwa tunaelekea tena kuzimu na kisha akaniuliza kama nilikuwa na hofu. Nikamwambia kuwa nilikuwa naogopa. Akasema, Roho ya hofu haitoki kwa Baba yangu, inatoka kwa shetani. Hofu itakusababisha ufanye vitu vitakavyo kupeleka kuzimu.  Bila imani ni vigumu kumpendeza Mungu na hofu ni kinyume cha imani. Nidhahiri hofu haimpendezi Mungu kwasababu huharibu imani ya mtu ya mtu ”.

Kwa muda wote tukiwa njiani tulikuwa tukitembea upande upande lakini baada ya kufika lango la kuzimu akanishika mkono wangu kwa muda wote tuliokuwa kuzimu. Nilikuwa na furaha kwasababu alinishika mkono na kwa kunishika aliondoa hofu yote ndani yangu. Sehemu hiyo ilikuwa bado inafanana na ya kwanza; hapakuwa na tofauti na sehemu ya kwanza. Kulikuwa na vijidudu virukavyo, minyoo, joto lililokithiri, harufu mbaya, mifupa, kelele. Kila kitu kilikuwa kama nilivyoona mara ya kwanza.

Mtumishi aishia motoni
Tuliingia lango kama lilelile tena akanipeleka kwenye moja ya makundi ya watu. Kulikuwa na watu wengi niliokuwa nawafahamu walipokuwa hai duniani. Watu walikuwa katika hali mbaya sana; walionekana wamefedheheka na uchungu mzito lakini kibaya zaidi walionyesha sura zisizo na matumaini.


Bwana akamwashiria mwanamke mmoja mwenye umri wa kati. Nilimjua kabla ya kifo chake kilichotokea kwa ajali ya gari mwanzoni mwa 2005. Nilishtushwa kumuona kuzimu kwani sote tulimjua kama mcha Mungu. Bwana akaniambia kuwa mwanamke alimpenda Mungu na Mungu pia alimpenda mwanamke huyo. Alinitumikia alipokuwa duniani, Aliwaongoza wengi kwa Bwana na alimjua Bwana vizuri. Alikuwa mwema kwa maskini na wahitaji; alitoa kwa ajili yao na aliwasaidia katika njia mbali mbali. Alikuwa mtumishi mzuri wa Bwana katika njia nyingi.

Maneno haya ya Bwana yalinishtua sana na zaidi nilipomuuliza kwanini akamwacha mtu aliyemtumikia vizuri aishie kuzimu. Bwana akajibu kuwa ijapokuwa alijua sana maandiko alikubali uongo wa shetani kuwa kuna dhambi ndogo na kubwa. Alifikiri dhambi ndogo haitamwangamiza kuzimu  maana  yeye   ni  mkristo.  Bwana  akaendelea   kusema,  Nilienda  mara  nyingi  na kumwambia aache alichokuwa akikifanya lakini mara nyingi aliendelea kufikiria kuwa dhambi hiyo ni ndogo sana na mwisho akachukulia kuwa maonyo niliyompa yalitokana na dhamiri dhaifu aliyokuwa nayo. Kuna wakati aliacha dhambi hiyo lakini baada ya muda akairudia huku akajishawishi kuwa maonyo hayo ni sauti ya kwake mwenyewe maana dhambi hiyo ni ndogo na haiwezi kumhuzunisha Roho Mtakatifu”.

Nikamuuliza tena Bwana anieleze  dhambi aliyoifanya mwanamke huyo, naye akanijibu kwamba, Mwanamke huyu alikuwa na rafiki yake Nesi katika hospitali ya Oshakati. Wakati wowote alipokuwa  mgonjwa  hakuwa  akilipia  kadi  ya  hospitali  kama  inavyotakiwa  bali  alikuwa anampigia rafiki yake simu na wanafanya mpango wa yeye kupata dawa kutoka kwenye zahanati. Rafiki yake alikubali kumfanyia hivi wakati wote”.

Hukumu yake ni kuwa:
·    alikubali uongo wa shetani juu ya dhambi ndogo na kubwa na hivyo kuikataa kweli yangu.
·    alimsababisha mwenzie kutenda dhambi ya kuiba kwa niaba yake.
·    lililo baya zaidi, alimhuzunisha Roho Mtakatifu. Hii ndio lilimpeleka kuzimu.

Haijalishi kama utaleta mamilioni ya nafsi kwa wokovu bado unaweza kuishia kwenda kuzimu kwa kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Ni lazima uangalie wokovu wa wenzio lakini uwe mwangalifu usisahau roho yako. Uwe makini na kila jambo unaloambiwa na Roho Mtakatifu. Baada ya Bwana kuyasema hayo akaniambia turudi.

Unayachukuliaje maneno haya?
Wakristo wengi waliosikia simulizi hii hupata maswali mengi. Wanajiuliza, Je kuhesabiwa haki, huruma na neema za Mungu hazina nafasi yoyote?. Na je unaweza kuupoteza wokovu baada ya kuupokea?”.
“Mbona neno hili lina ukali sana? Mungu anaweza kuwa katili hivyo?”.

Kama nilivyosema mbeleni mimi sifundishi theolojia. Ninasema tu mambo ambayo Bwna alinionyesha na kunifundisha. Nakuomba uangalie Biblia yako vizuri kwa majibu. Hebu angalia vifungu vifuatavyo halafu ujiamulie.
Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. (1Wakorintho 9:27)
Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? ( Warumi 6:1-2)
Basi dhambi isitawale ndani ya mioyo yenu ipatikanayona mauti, hata mkazitii tamaa zake
(Warumi 6:12)
Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. Bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.    (Waebrania 10:26, 27)
Je  naweza  kuishia  kwenda  kuzimu  baada  ya  kumtumikia  Bwana  na  kuwaongoza  wengi  kwa
Kristo? Jiamulie mwenyewe.


Kutotii
Jumatatu tarehe 06/03/2006, niliamka saa kumi na moja na nusu alfajiri. Nilipoanza kuomba nikaona kuna nguvu za Mungu za ajabu juu yangu. Mwili wangu ulikuwa dhaifu na nilikuwa natetemeka. Nguvu kama za umeme zilikuwa zinapita mwilini mwangu.

Mchana  nilipokuwa  nimelala  nikaonmwangmkubwa  wa  ajabu  ukikijaza  chumba  chote. Nikaona  vitu  vidogo  vyeupe  vyenye  umbo  la  mviringo  vikiniangukia  kammvua  na  kuingia mwilini. Kisha nikaona wingu la kitu kama ukungu likishuka, kukijaza chumba chote na pia kuanza kuingia mwilini mwangu. Nikamwona Yesu akinijia akiwa katikati ya wingu lile la ukungu na akaketia kiti chake kandokando ya kitanda changu. Sijui kiti hicho hutoka wapi ila huwa kinatokea akiwa tayari kukaa. Kiti chenyewe kimeundwa na dhahabu tupu, kuna nyota ya shaba kwenye kila mguu wa kiti hicho. Mahali pa kujiegemezea pamewekwa pia nyota kubwa ya shaba na kila mguu wa kiti hicho kuna magurudumu ya mviringo.

Yesu  akaninyoshea  mkono  kunisalimia.  Akaniambia  niinuke  kwa  kuwa  MUDA  UMEISHA. Akanivuta kwa mkono na nikakaa juu ya kitanda. Akaniambia, Victoria tuombe. Akaomba kwa lugha ambayo sikuelewa. Nilichoelewa pekee ni neno ‘Amina’. Akaniuliza nilichokuwa naona. Watu walikuwa wakiingia kazini. Nikaona vile vitu vidogo vya mviringo vikiwaangukia kundi la wale  waliotangulia  kufika mahali  pao  pa kazi. Waliofika  baadaye walipata mvua ya vitu vile imekatika. Jambo hili pia nikaliona kanisani, waliotangulia waliangukiwa na vitu hivi vyeupe lakini waliofika baadaye hawakuvipata.

Yesu  akaniuliza  kama  naelewa  maana  ya  maono  hayo  nami  nikamjibu  kuwa,  Sielewi.  Basi
akanieleza,
Maono hayo yana maana kuwa kila mahali unapostahili kufika kwa wakati fulani, na unaujua wakati huo, kuna Malaika wanawagawanya baraka, kwa muda ule. Anayewahi anapata baraka zile anayechelewa anazikosa kwa kuwa Malaika hugawa baraka kwa muda tu. Vitoria nataka nikuonye kwa kuwa unachelewa kwenda kazini na unachelewa zaidi kwenda kanisani. Elewa kuwa  siku  ulizochelewa  bila  sababu  umekosa  baraka  zako  za  siku  hizo  milele.  Baraka  hizo haziwezi kukurudia. Victoria ni lazima uache jambo hilo na usirudie pengine uwe na sababu nzuri”.

Aliponiambia hivyo nilitamani kumkimbia au  kumpa sababu nzuri kwa kosa hili. Nikamwambia nilikuwa  na  tatizo  la  kulala  sana  lakini  akaniangalia  moja  kwa  moja  usonna  kusema  kuwa nilikuwa na tatizo la kurudi tena kitandani baada ya kuamka, nilikuwa naangukia majaribu ya kutaka kulala dakika zingine chache.



Yerusalem Mpya
Baadaye akaniambia, “Amka twende MUDA UMEISHA na kuna vitu lazima kuvifanya. Akanipeleka mahali sijawahi kufika, barabara yenyewe ilikuwa mpya kwangu. Tukafika kwenye bustani yenye maua mazuri na miti mizuri ya kijani kibichi; hakuna kitu duniani cha kulinganisha na uzuri huu. Tukakalia kiti cha dhahabu kilichokuwa kwenye bustani hiyo nzuri.

Tulipokuwa tumekaa, Yesu aliniashiria mbele kwa kidole chake na kusema, Victoria angalia, je wauona mji ule?”. Nilipoangalia nikaona mji mkubwa uliokuwa na mwanga mkubwa. Mji huo ulikuwa mzuri kupita maelezo. Lango lake lilikuwa la dhahabu huku liking’aa ajabu, na mtu mwenye umri mkubwa alikuwa amekaa pale. Mtu huyo alikuwa na ndevu na nywele nyeupe. Nilikuwa nimemwona hapo mbeleni na nilipomuuliza Bwana, akaniambia kuwa ni Abrahamu, baba wa Imani.

Niliona barabara nyingi ndani ya mji ule zilizojengwa kwa dhahabu. Kulikuwa na majumba ya
ghorofa yalokuwa yaking’aa kama dhahabu. Mngao wa jiji lile kwa kweli hauelezeki. Yesu akanigeukia na kuniuliza, Unafikiria nini juu ya mji ule?”

Nilijibu kuwa ni mji mzuri na nataka niende huko. Yesu akasema, Nitakupeleka huko ukiendelea
kuwa  mtiifu,  maana  ndiko  iliko  nyumba  yako.  Ishi  kwa  uaminifu  ukishindwa,  nyumba  yako


itakaliwa na kunguru na bundi. Itakuwa uwanja wa pepo wabaya. Hata hivyo usihofu, kwasababu niko pamoja nawe, wewe kuwa mtiifu tu. Asiyetii nyumba yake itakuwa makazi ya bundi na uwanja wa mapepo wabaya.

Yesu Kristo kweli yupo na anatupenda kwa upendo usioelezeka. Hitaji kubwa la moyo wake ni wanadamu tuchaguwe uzima ili tukae nae milele.
Moyo wake unaugua kwa ajili ya watu wanao kufa na kuishia kuzimu kwasababu ya kuuacha wokovu aliowapa na kuchagua mauti.




Haijalishi umeokoka au haujaokoka neno moja tu ukumbuke ni kuwa: MUDA KWA HARAKA SANA UNAKWISHA.




6 Messages to the Church 
Miraculous Healing and Divine Invitation to Heaven 


Introduction:
In May 2006, a servant of God was brought to Heaven to meet with the Lord Jesus and receive a revelation of 6 messages.  Brani Duyon @ Efendie, age 52, a Dusun ethnicity.  He serves in the Borneo Evangelic Church, Kota Belud, Sabah (in East Malaysia) as an Elder.  He had served as Pastor in Melangkap Baru, Kota Belud, and later became the Church Leader at the SIB Bayayat from 2005-2006.


On April 21st, 2006, my wife and I went to West Malaysia to attend the wedding of our son.  Unfortunately after one week, I had a sudden stroke.  I was immediately brought to the medical centre in Malaya University where the doctor examined me.  He told me that there was a rupture of blood cells in my brain and I
immediately needed to get an operation.  
I was in comma for one week after the operation and in intensive care unit for 1 more month. There were many servants of God who came to visit and pray for me, including the former SIB Sabah President - Pastor Taipin Melidoi, his assistant - Pastor Datuk Arun Selutan, and also Pastor Michael.
I once dreamed of a heavy rain pouring on me.  I interpreted this dream as the answers to the Pastors who had prayed for my recovery.  Praise God, with His power I recovered sooner than expected.  
One midnight, during the third week of May 2006, I felt very strange.  I could not go to sleep, while the other patients had slept soundly.  During this time, I had my mind only on Jesus.  I remembered in Isaiah 43:26 “Review the past for me, let us argue the matter together; state the case for your innocence."  I kept thinking of these words because I wanted to focus my mind only on the Lord
Jesus.  I could feel the strong presence of God at that time.  

Then I started to pray in the spirit.  After praying, I tried to sleep again but I just could not.  Then I leaned back in my bed.  Suddenly I felt as though someone was tapping on my back and stroking on my head.  This happened for a while.  I felt something amazing flowing into my body.  I believed it was a father’s love to his child.  I wondered who this person was.  When I turned to face him, I was amazed to see that he was a young and handsome man, well-built, tall with a long hair down to his neck.  And he was wearing a white dress.  I asked him, “are you the Lord that I have been thinking of?”  He only shook his head.  Then I asked again, “if not then who are you?” At last he started talking to me “I am a messenger from Heaven.  Jesus told me to come to you for good news.”
Now I realized that he was the Angel of God, so I asked him, “what is the good news you want to tell me?” He replied, “tonight you will go to Heaven”.  Immediately I felt very calm and peaceful even though my body was sick.  I felt as if I did not have any pain.  I had fully recovered from my sickness the moment the Angel told me that I was going to Heaven.  Then I said to the Angel, “I’m ready to follow you to heaven.  I can’t wait to see my Lord.”
While we were walking I saw my earthly body was left on my bed.  After we walked out of the hospital, I saw an amazingly big and tall horse.  “We will ride this horse,” said the Angel.  The Angel helped me onto the horse, since it was so tall.  Then I asked the Angel, “can we go to Heaven by riding this horse?” The Angel then assured me, “of course, don’t be afraid and worried.  Have you read the Word of God about Elijah who was taken up to Heaven by God?” I told him “yes, I read it before.  The vehicle that brought him was a chariot of fire, pulled by horses of fire.” “That’s right, and that is one of the horses that we will ride now,” said the Angel.

At first we went slow, but after about 100 meters the horse accelerated to a very high speed and I felt as if we were hit by a hurricane.  Then I saw the horse was already flying.  We crossed many mountains with ease, flying with God’s power.
Then we reached to a very big field with green grass – it was perfect, with not one dry blade of grass. (Psalm 23:2 “He lets me rest in fields of green grass and leads me to quiet pools of fresh water").

After the horse stopped, we went down and began walking.  
I could see the Kingdom of God right before my eyes.  As we were walking on the field, I heard a bell rang.  Then I asked the Angel “why does the bell ring?” He said “the bell is a sign that someone has come.”
We continued walking to the end of the field, while the bell was still ringing.  I saw a very beautiful house, on its top was a red light, like a traffic light.  On this light I saw the number “51”.  I asked the Angel what the number meant.  He said, “what is your age now?” During this time I was 51 years old.  “Then that number is your age, so is your house number too,” the Angel told me.  I felt so happy and peaceful to see what God has prepared for me in Heaven.  I saw many houses which are already prepared by Jesus for His children who believe and follow Him.

We continued walking to a very huge house, with many people inside.  I believe they were the holy people that God have chosen.  They were praising God.  I saw Jesus was sitting on His throne while all the people were praising and worshipping Him.  They praised Him with all their hearts, they danced, they lifted their hands and they bowed to their knees.  Deep in my heart I said, “if only people on earth praise and worship Him like this, God will be very pleased.” 
I saw many people were crying while praising God.  Jesus smiled while watching how devoted they were to worship God.  They lifted their hands towards Jesus and Jesus was blessing all of them.
After the service finished, Jesus walked among them and wiped off their tears.  Then I remembered the verse in the book of Revelation, “there will be no more death, no more grief or crying or pain".  
The Angel brought me in to Jesus.  The Angel spoke to Jesus “Lord, this is the son that You have chosen to come here.” Jesus then said to me, “Great! My son you have come today”.  Then Jesus hugged me and it made me so happy and peaceful that I cried.  My soul jumped with joy because Jesus Himself hugged me.
The Angel then said, “Lord, I went to His house on earth when he was sick, nevertheless He is now better.” Jesus replied, “yes, I heard and saw what happened to him.” The Angel continued, “during that time, I heard his wife pray for Your help.  She prayed: “Lord, help us, please don’t take him now because we are not ready for him leaving us yet.” That was her prayer, Lord.” Jesus then said, “I know everything.  His wife is a God-fearing woman.  She is faithful to Me and diligent in prayer.”

Then my soul cried again thinking of my wife’s faithfulness to God.
Then God spoke to me, “My son, you will go back to Earth, because it is not your time yet to be here.  There is a lot of work for you to do when you go back there.  You will be very busy to serve Me.” Then I replied, “Lord, please don’t ask me to go back, because I am very peaceful to be with You here.  I feel happy to be close to You Lord.  Please, I don’t want to go back.”  From His face, I can tell Jesus became disappointed.  Then I begged Him for His forgiveness because I had disappointed Him.  I said, “Lord, I’m ready to go back to Earth but please help me Lord, give me strength, and take care of me wherever I go.  Be with me Lord.” Jesus then said, “yes, don’t worry, wherever you go to serve Me, I will always be with you.” 
Jesus had messages for me to bring to Earth.  He wanted me to tell these messages to the children of God on Earth.  “These messages are very important for them to know”, said Jesus.  I was told that I would be very busy getting out these messages.  Jesus also wanted me to share my Heavenly experiences to all the children of God so they will be blessed and renew their strength to follow Him.
Jesus spoke to me, “when you go back to earth tell all My children these messages” (There were SIX MESSAGES which Jesus had given to me):

FIRST MESSAGE:
“Tell My children, they must believe in Me with all their heart, their strength, and their mind.  Those who are worried and doubtful will not get in here,” said the Lord Jesus.

SECOND MESSAGE:
“Tell My Children, they must be faithful to come to the Church service, because that is the time when I will shine over their faces and they will look for My face.  I will be very pleased to see My children worshipping at Church,” said the Lord Jesus

THIRD MESSAGE:
“Tell My Children, they must be faithful to pray, do My will, and live with My words,” said the Lord Jesus

FOURTH MESSAGE:
“Tell My children, they must be obedient to give tithes and offerings," said the Lord Jesus. (While Jesus was giving me this message, He said “My child, look there” He showed me beautiful houses which are ready for His children.  “My child, these houses are ready, I prepared for all My children that believe and are obedient to Me.” Then He showed me incomplete houses.  I asked“Lord, why are these houses not yet completed?” The Lord Jesus said “My child, these houses
belong to My children that are not generous giving tithe and offerings.  These houses will be ready and completed after My children give more tithes and offerings in My House.”
 
FIFTH MESSAGE:
“Tell My children, they must put in prayer all their wealth to Me for protection and blessing while they are still on Earth, so that when I come to Earth for the second time, they will not be attached  to their Earthly wealth.  Remember the story of Lot wife,” said the Lord Jesus.

SIXTH MESSAGE:
“Tell My children, they must be ready and alert, because I will be coming soon.  Sooner than people expect!”  said the Lord Jesus, (Jesus’ coming is not known but the rupture will surely take place.  Lord Jesus will come soon!!!)
While Jesus told me the sixth message, He showed me the sky, it was all clear and no clouds.  I saw Jesus opened His hands to Earth and He spoke “I am ready to take My children.” Then I saw many people in white robes flying up in the sky to meet Jesus.  They were gathered to the left and right side of Jesus.  Many people who believe in Jesus were ruptured.  Moreover, I saw all members of many families were being ruptured.  I could see the husband and wife with their children flying up towards Jesus.  I felt so peaceful to see this sight.  
Then Jesus insisted, “look down”.  Jesus then showed me the situation on Earth, it was very chaotic. There was no peace on Earth during that time.  I saw people were running all over the place and shouting.  Parents were looking for their children and youths were looking for their parents.  
Jesus showed me the Church in my hometown.  I felt so sad, because there were some people who were left behind.   Jesus then said to me, “be faithful to Me.  You must convey all things that you have seen and heard to My children on Earth.”
Then the Angel took me to Earth on the same horse we rode before.  We got to Earth very fast.  Then the Angel took me back to the hospital.  While I was looking at my earthly body, my spirit immediately went back into it.
I noticed that my body had fully recovered from the sickness. 
Praise God for His power!
I remember that when I was in Heaven my body looked like as it did when I was young.

That is my testimony of meeting with the Lord Jesus in Heaven. 



No comments:

Post a Comment