Saturday 31 December 2016

KAZI YA ROHO MTAKATIFU



INGIZO:

A. Ulimwengu wetu una sehemu mbili, yaani ile ya kimwili na ile ya kiroho, yaani ile ya dunia hii na ile isiyo ya dunia hii. Lazima kila mwanafunzi Hhodari azione pande hizo mbili tofauti katika kuishi kwetu. Upande ule moja hauwezi kujibu badala ya ule mwingine, wala ule mmoja hauwezi kutwaa mahali pa ule mwingine.
B. Roho Mtakatifu wa Mungu alifanya kazi pan de zote za muumbo wa ulimwengu. Upande wa kimwili na upande wa kiroho vilevile.
C. Kazi ya Roho Mtakatifu ilifunika muumbo wa kimwili na ule wa kiroho vilevile. D. Kuonyesha kazi ya Roho Mtakatifu katika muumbo wa kimwili na wa kiroho.
I. KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA MUUMBO W A KIMWILI: A. Uungu katika muumbo.
1. Mungu Baba alikuwa ameanzisha, akaandaa, akatawala.
a. Yer. 51:15 - ameumba kwa uweza wake, hekima, na ufahamu wake ... kwa hiyo alikuwa akiweza yote na akijua yote.
b. Zab. 29:4 - Mungu alisema, ulimwengu akawa, Mwa. 1:3.
c. 1 Fal. 8:27 - "Mbingu na mbingu za mbingu" hazimtoshi. Yeye ndiye aliyepo mahali pote, Zab. 139; Yer. 23:24.
2. Neno aliumba vitu vyote - Yn. 1:1-3; 1 Kor. 8:6; Kol. 1:16-17; Ebr. 1:2; Mwa. 2:3. Neno lililonenwa ndilo mtendaji wa Mungu katika muumbo.
3. Roho Mtakatifu alikuwako katika muumbo - Mwa. 1 :2. "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu" Tohu na Bohu, 'ghasia na buruga bila mpango wala ularatibu na sehemu mbalimbali" (Katika Komentari ya Clarke).

"lkatulia" - Merachepheth, "Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji ... neno hilo ni kama mfano wa kuku aatamiaye akiatamia mayai au akilisha vifaranga wake." (Katika Komentari ya Clarke).

“Roho" - Ruach, katika A. J. limetafsiriwa kwa Pneuma, "Roho Upepo .. " Hapa neno lile "wa" katika "wa Mungu" huonyesha kwamba ndiye mali ya Mungu na uhusiano wake pamoja na Uungu. na bila shaka huyo ndiye Nafsi ya Tatu wa Uungu, Yn. 3:8, pia Mdo. 2:2.

B. Mtakatifu aliweka utaratibu wa ulimwengu wa kiriiwili. Kuweka utaratibu, - kutengeneza au kusimamia sehemu zinazotegemeana; kupanga sehemu zisizo na utaratibu.

Neno lile la Kiingereza "Universe" ni kutoka lugha ya Kilatini: "Unus" ni kama "moja", na "vertere, versum" ni kama "kugeuka"; kwa hiyo "universe" ni kama "kugeuka kuwamoja".
1. Maneno matatu ya Kiebrania katika Mwa. 1-2: muumbo, utengenezaji, na ufanyaji katika mwanzo.


a. "Bara", "kuumbwa", "kUita katika kuwako, kufanya kuwako ambako zamani hakukuwako na kitu cho chote." (Boles) "Neno hilo hudhihirisha chanzo cha kuwako kwa kitu, . au kutokea kwa kutokuwako katika' kuwako. Maana yake ya kwanza siyo kudumishawala kufanya upya kwa vitu vilivyokuwako zamani, kama wengine wafikirivyo, lakini ni muumbo wa asili hasa" (Katika Komentari ya Clarke) Latumika kwa muumbo wa mbiugu na nchi - Mwa. 1: 1. Latumika kwa muumbo wa viumbe vyenye uhai katika bahari na katika anga - Mwa. 1:21.

Latumika kwa muumbo wa: mwanadamu - Mwa. 1:27.

b. "Asah", "kutengeneza (vitu na vitu vya asili vilivyokuwako kutoka zamani)"; Iatumika kwa muumbo wa mwanadamu, Mwa.
1:26. Sehemu za mwanadamu zilikuwa zimetengenezwa kwa vitu vilivyokuwako kabla yake, mwili wake.
c. "Yarsar", "kufanyiza, kupasha sura" - latumika kwa mwanadamu
- Mwa. 2:7.
d. Webster ameeleza tofauti ya maneno hayo katika lugha ya Kiingereza (neno la "kutengeneza") "'kutengeneza', ambalo ni neno litumikalo sana, halitumiki tu kwa kufanya kazi kwa mikono, vyombo, n.k., bali kwa akili, na Mungu vilevile; 'kufanyiza'; neno hila ladokeza ya kwamba kitu kile kilichofanyika kina umbo, sura, muundo wake wa pekee n.k."
2. Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu alivyovitengeneza vitu, akivipa sura, uhai, na nguvu ya kuzaa. Kutoka hali ya ukiwa na utupu, jinsi tusomavyo Mwa. 1:2, Roho Mtakatifu alivitengeneza vitu vyote kwa mpango wa utaratibu kamili.
C. Roho Mtakatifu alltoa sheria za kuendeleza ulimwengu.
1. Vitu vyote vilianzishwa kwa ajabu, kwa muumbo, lakini viliendelezwa kwa sheria ya asili. (Baadaye itaonekana jinsi ufunuo wa mapenzi ya Mungu ulinganavyo na hayo, mapenzi ya Mungu yalijulishwa kwanza kwa ajabu, kisha yakaendelezwa kwa sheria.)
a. Ayu. 26:13 - Roho Mtakatifu alizipamba mbingu. "'Kupambwa' kwa mbingu, labda maana yake ni kuweka sayari za angani mahali pao pa kufaa, na kudumisha kwake huzunguka katika miuda ya mwenendo wao angani wakati wote ikiwapo. Kazi hii hufanyika na Roho Mtakatifu, na huendelezwa na Roho vilevile." (Boles, uk.
40), Mwa. 1 :11, 22.
b. Zab. 104:30 - Roho Mtakatifu akagua jamii ya Isa. 32:15.

Kuwa mahali pote. Kwa hiyo, po pote sheria za asili zilizopo, ndipo Roho Mtakatifu yupo. Mimea na miti.
c. Zab. 139:7-10 - Roho Mtakatifu ana uwezo wa
2. Mwanadamu alikuwa ameanzishwa kwa ajabu, lakini aendelea kuzaliwa kwa sheria ya asili.


a. Mwa. 1 :26-27 - Alifanyika, akaumbwa kwa mfano wa Mungu. b. Mwa. 2:7 - Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi.
c. Kut. 31:3 - mwanadamu amejazwa "roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina."
d. Ayu. 32:8 - "Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, na pumzi ya Mwenyezi huwapa akili."
e. Ayu. 33:4 - "Roho ya Mungu imeniumba."
f. Mwa. 1 :28 - Mwanadamu amepewa sheria ya kuzaa, yaani kuzaa wengine kwa sura yake wenye tabia na asili hizo zile zile.

II. KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA MUUMBO W A KIROHO: A. Baba katika utaratibu wa ukombozi.
1. Mungu Baba alikusudia utaratibu wa ukombozi Rum. 8:28-29; Efe. 1:3 n.k. "Kujua tangu asili," "pro-ginosko", (kwa Kiyunani) kutoka "pro" = "tangu asili", na "ginosko" = "kujua", kwa hiyo ni "kujua tangu zamani, kabla haijatokea", m.y. kujua kabla ya muumbo wa kimwili.

"Kuamuru tangu asili" = "pro-horizo" (kwa Kiyunani), kutoka "pro" = "tangu asili", na "horizo" = "kuweka mipaka", kwa hiyo ni "kuweka mipaka tangu asili", kabla ya muumbo wa kimwili.
2. Kol. 2:9 - Utimilifu wa Mungu ulikuwapo katika Kristo. Kwa hiyo, ukamilifu wa Baba ulikuwapo katika Kristo "Uungu" = "theotes" (kwa Kiyunani) = "Diety" (kwa Kilatini), m.y. "hali ya kuwa Mungu", johari ya Uungu (Thayer, uk. 288). Neno lile la "Uungu" au "Umungu" hueleza yale yale kuhusu Utatu, kama maneno yale ya "utu" na "utoto" hueleza kuhusu hali ya kuwa mtu au mtoto, yaani ni nini hasa imfanyayo mtu kuwa mtu, aumtoto kuwa mtoto.
3. Yesu amezaliwa na Mungu - Yn. 1:18; Mdo. 13:33.
4. Mungu Baba alimtuma Kristo duniani - Rum. 8:3.
5. Mungu alikuja ndani ya Kristo - 2 Kor. 5:19.
B. Kristo alikuwa mtendaji katika kutimiliza utaratibu wa ukombozi.
1. Mt. 1:23 - Alikuwa Imanueli, "Mungu pamoja nasi".  Uungu
uliofanyika mwili. "Kuwakatika mwili", "kuvikwa kwa mwili, au kwa hali na sura ya kimwili; kufanyika mwili kwa sura ya binadamu" - Webster.
2. Fil. 2:6-7 - Yesu alikuja duniani kwa mapenzi yake mwenyewe.
3. Yn. 4:34 - Yesu aliwafunulia wanadamu mapenzi ya Baba.
C. Roho Mtakatifu alitengeneza na kufunua utaratibu wa ukombozi, Yn. 14:16-
18; 14:25-26; 15:26-27; 16:7-16 .
1. Lk. 1:35 - Alimfunika Mariamu kama kivuli, akishirikiana katika
Kufanyika mwili.
2. Mt. 1:18, 20 - Mariamu a1ikuwa na mimba kwa uweza wa Roho
Mtakatifu.
3. Kol. 2:9 - Utimilifu wa Uungu katika Kristo.
D. Roho Mtakatifu alitoa Sheri a kwa Ufalme wa Kiroho.
1. Mt. 10:20; Yn. 14:26 - Alisema kwa vinywa vya mitume.
2. Yn. 15:26; 16:7-15 - Aliwafunulia mitume mambo fulani.


3. 1 Kor. 2:13 - Mitume walikuwa wakiandika, wakati wakiongozwa na
Roho.
4. 1 Kor. 2:13 - Mitume walikuwa wakinena kwa njia ya Roho.
E. Yatokanayo na hayo: Ulinganifu wa tabia za muumbo wa kimwili na wa kiroho.
1. Nafsi zile zile upande wa kimwili na kiroho.
2. Utawala ule ule katika zote mbili.
a. Mungu Baba alianzisha na kupanga zote mbili.
b. Mungu Mwana, Kristo kama Neno, alikuwa mtendaji wa zote mbili akizitimiliza zote mbili.
c. Mungu Roho Mtakatifu alitengeneza akakamilisha na kuziendeleza zote mbili .
d. Kwa hiyo, kuna upande wa kimwili na upande wa kiroho, ambazo zote mbili zimetengenezwa na Roho Mtakatifu kufuatana na mapenzi ya Baba, zikiwa zimetimilizwa na Mwana.

AZIMIO:

Twaona ya kwamba madhumuni yetu yamefafanuliwa wazi kwa kutosha kuwa ni kweli, yaani Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kaz;i katika muumbo wa kimwili na kiroho vile vile.

No comments:

Post a Comment