Saturday 31 December 2016

VIPAWA VYA MWUJIZA VYA ROHO MTAKATIFU



INGIZO :

A. Vipawa vya mwujiza vya Roho Mtakatifu vilitolewa na Mungu kwa Mitume; viliweza kugawanywa katika kanisa 1i1e la zamani kwa njia ya "Kuwekewa mikono" ya Mitume; vilikoma wakati makundi hayo mawili yalipokufa na ufunuo wa maandiko ulipokuwa tayari.
B. Kuonyesha hali ya vipawa vya mwujiza; kuchunguza jinsi vilivyapoke1ewa na jinsi vilivyogawanywa; kuonyesha vipawa vya mwujiza vilidumu kwa muda gani.
C. Katika masomo yetu mpaka sasa, tumeona ya kwamba "kipawa cha Roho Mtakatifu" katika Mdo. 2:30 kilikuwa Roho Mtakatifu mwenyewe. Tuliona vile vile kwamba kili- kuwa ahadi ya kuenea po pote kwa wote waaminio na kubatizwa wapate ondoleo la dhambi. Tuliona kwamba Ubatizo wa Roha Mtakatifu uliwafikia Mitume tu, isipokuwa Kornelio na nyul11ba yake vile vile, ili ionyeshwe wazi kwal11ba Mungu amewapokea mataifa jinsi alivyowapokea Wayahudi. Mdo. 11:17-19. Sasa tutaingia somo juu ya vipawa vya mwujiza vya Roha Mtakatifu, jinsi vitumikavya, jinsi vipatikanavyo, na jinsi vikomavyo.

I. KULIKUWA NA "KIPAWA CHA MWUJIZA" CHA ROHO MTAKATIFU:

A. Watu "waliowekewa mikono" ya Mitume walipokea nguvu ya mwujiza. Mdo.
6:5-6, 8; 8:6-7, 13, 17-19; 19:1-7; Rum. 1:11.
B. Lakini wale ambao Mitume "waliweka mikono" juu yao, hawakuweza kuwagawanyia wengine kipawa hiki!
1. Filipo alikuwa mtu wa aina hii. Mdo. 6:5-6; Mdo. 8:7, 13.
2. Mitume walihitajika wagawanye kipawa hiki. Mdo. 8:18.
3. Lakini hata Filipo alikuwa na uweza akawabatiza, Mdo. 8:12-13; kwa hiyo walipokea "kiwapa cha Roha Mtakatifu" kama ilivyo Mdo. 2:38.

Maangalizi:

1. Yaonekana ya kwamba "kipawa" katika Mdo. 2:38 hakikuwa cha mwujiza.
2. Wale ambao Mitume waliweka mikono juu yao, wakati walipoweza kutenda miujiza, hawakuweza kuwagawanyia wengine hiki.

II. KIPAWA HIKI CRA MWUJIZA KWA NJIA YA "KUWEKEWA MIKONO" YA MITUME KWA WATU BINAFSI FULANI.

A. Mitume "waliweka mikono" juu ya haa wafuatao:
1. Wale Saba, Mdo. 6:5-6.
2. Wale Wasamaria, Mdo. 8: 14-21.
3. Wale Waefeso, Mdo. 19:1-7.
4. Wale Warumi, Rum. 1:11, n.k.


B. Maonyesho ya mwujiza yalitokea.
1. Kunena kwa lugha ya mwujiza yameorodheshwa, 1 Kor. 12:1; 12:4;
12:8-11; I Kor. 12:28-31. (vipawa tisa vya mwujiza kwa jumla).

Maangalizi:
1. Roho Mtakatifu hakuto1ewa kwa kitendo ki1e cha kuwekea mikono ya
Mitume, bali ilikuwa i1e asili ya mwujiza tu iliyogawanyika.
2. Hii haikuweza kupitishiwa kwa ye yote mwingine.
3. Miujiza ilishuhudiwa kila mara wakati Mitume walipogawanya kile kipawa cha mwujiza.
4. Roho Mtakatifu kama kipawa alikuja kwa njia ya kuitii injili; Mdo.
2:38; maonyesho ya mwujiza yalitokea kwa mikono ya Mitume tu. III. KlLE " KIPAWA CHA MWUJIZA" LAZIMA KIMEKOMA.
A. Kama kilitokea kwa mikono ya Mitume tu basi bila shaka haiwezekani kukitazamia siku hizi - kwa hiyo siku hizi hakuna ushuhuda wa kweli wa miujiza ya Mitume na Kanisa lile la zamani.
B. Biblia yaonyesha jinsi miujiza ilivyotumika, Mk 16:16-20; Ebr. 2:1-4.
1. Kuthibitisha neno lao.
2. Neno limekwisha thibitishwa.
3. Kwa hiyo hakuna haja na miujiza siku hizi.

Maangalizi:
Kwa njia hii, na kwa njia hii tu, yawezekana kujua kwamba msemaji alifundisha ukweli.

C. 1 Kor. 13:8-12, mistari hii yafundisha wazi komo la mambo ya mwujiza:
1. Unabii - lugha - maarifa - zote zitakoma. Hizo zilikuwa za mwujiza, 1
Kor. 14.
2. Ijapo ile iliyo "kamili". Katika lugha ile ya asili ya Kiyunani, neno lile
"kamili" lipo katika mfano wa kuonyesha kwamba ni kitu hasa, siyo mtu ..
3. Maelezo yaliyotolewa na Paulo yaonyesha kwamba ile "kamili" ndiyo ufunuo uliomalizika, mst. 12. Pia, neno lile "kamili" lina maana ya kuwa "zima" au "pevu".

Maangalizi:

1. Kama ya Mwujiza yangewezekana au yangetokea leo, wateteaji wangevunja 1 Kor. 14 vibaya!
2. Wakati kanisa lilipokuwa katika hali ya uchanga, lilihitaji "misaada hii ya pekee" '- lakini hili siyo lazima siku hizi. Ufunuo uliomalizika watukabidhi yote tunayohitaji, Yud. 1:3; 2 Pet. 1:3.

Swali :


Nini inayohusu "mambo ya mwujiza" yashuhudiwa katika dini siku hizi? AZIMIO:
Mungu alipowaumba mwanamume na mwanamke, hii ilikuwa imetokea kwa mwujiza;
baadaye sheria ya asili ilianza kazi.

Mungu alipoliunda kanisa liwepo, aliyatumia mambo ya mwujiza ili alianzishe na kulisaidia kanisa katika uchanga wake. Mwishowe sheria iliyokuwa imefunuliwa ilianza kazi: kwa hiyo madhumuni yetu ni ya kweli.


UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

INGIZO :

A. Mungu alitenda miujiza akauweka Ubatizo wa mwujiza wa Roho Mtakatifu. B. Kuonyesha Ubatizo wa mwujiza wa Roho Mtakatifu. Kuwaonyesha wale wa1ioupokea ubatizo huo. Kuonyesha kusudi la Ubatizo wa aina hii.
C. Kwa sababu wasiwasi na mashaka mengi yametokea katika jambo hilo, ni muhimu hasa tulizungumze swali hilo na kuyapeleleza Maandiko ili tupate ukweli katika jambo hilo.

I. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU: A. Ile "ahadi" ya Yohana, Mt. 3:11.
B. Ile "ahadi" ya Kristo, Lk. 24:48-49.
1. Iliwabidi "kungoja" katika mji wa Yerusalemu.
2. Iliwabidi kupokea "uwezo" utokao juu.
3. Iliwabidi "kushuhudia".
C. "Agizo" limetolewa mara ya pili, Mdo. 1:2-4. D. "Uwezo" umeto1ewa mara ya pili, Mdo. 1:5.

Maangalizi:

1. Kama huwezi kuyakinia kuhusu neno lile la Yohana katika Mt. 3: 11, ni nani anayesemwa, Yesu kwa "kusema maneno yake tena" na kwa "kuyaeeza" mbele ya Mitume, aeleza wazi kwamba ndio "Mitume tu" wanaohusika.
2. Wale waliopokea ahadi ile, waliupokea "uwezo" vile vile. Nani walioupokea "uwezo"? Mdo. 2:1-4, yaonyesha kwamba ni Mitume "tu" walioupokea "uwezo" wa kusema kwa "lugha", 2:13. Petro na wale kumi na mmoja wengine, 2:14. Pia fikiria neno lile "wao" katika Mdo. 2:1 na Mdo. 1:26. Ni wazi kwamba ndioMitume wa1iohusika.
3. Tangu wakati u1e tu Mitume "wa1ipoweka mikono yao" juu ya mtu, tunazo habari kwamba Mitume waliitenda miujiza, 2:43; 3:3; 3:6; 4:33;
5:12; 5:15-16; 6:6, 8.
4. Mitume wa1ikuwa mashahidi wa pekee, Mdo. 1:22, pia Mdo. 1:26 "akahehsabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja"; "sisi sote tu mashahidi wake", Mdo. 2:32; wasikilizaji waliwasihi Mitume walipowau1iza "watendeje", Mdo. 2:37. Hiyo ndiyo itimilizayo amri ya Yesu ya kusema, "ngojeni", "pokeeni uwezo", "shuhudieni".

II. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU ULITOKA MBINGUNI, NILIKUWA WA KUONEKA NA WA KISIKILIKA :

A. Ubatizo waRoho Mtakatifu ulitoka mbinguni hasa, ukakabidhiwa kwa utumi wa binadamu.
1. "Mungu amekimwaga kitu hiki".


2. "Mnaehokiona sasa".
3. Na "kukisikia,” Mdo. 2:33.

Maangalizi:
1. Yalikuwa mafafanusi ya1iyosikilika, 2:2. Kitu fulani kilioneka; kwa hiyo ya1ikuwa mafafanusi ya1iyooneka, 2:3. Kitu fulani kilitendeka; walianza kusema kwa kwa 1ugha (lugha, Mdo. 2:7-12; "lugha zetu wenyewe").
2. Hii siyo yale mathubutu yaliyo dhahiri katika "ahadi" ile ya Mdo. 2:39. Yale "ya1iyoahidiwa" na Yohana na Yesu, yakapokelewa na Mitume, siyo yale "yaliyoahidiwa kwa waamini wote. Siyo wote waliokuwa na kipawa cha lugha, 1 Kor. 12:10; 12:30, kwa hiyo "ahadi" mbili tofauti zahusika, 1
Kor. 12:29-31.
3. Wote "waliobatizwa katika Roho Mtakatifu" ndio wale waliosema kwa lugha, Mdo. 2:1-4; 2:6; 2:8; 2:11; 10:44-47. Laldni kulikuwa na wengine waliosema kwa kwa 1ugha bila kubatizwa katika Roho, Mdo. 19:1-6;
1 Kor. 12. Kwa hiyo Mdo. 2:39 hauhusu Ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa sababu, kama ingekuwa hivyo, basi wote wangesema kwa lugha; lakini Paulo akisema, "Je, wote wananena kwa lugha?", anaonyesha wazi kwamba sio wote. Lakini wote wameahidiwa kipawa cha Roho Mtakatifu; kwa hiyo ni wazi kwamba ahadi ya Roho Mtakatifu haifuniki Ubatizo wa Roho Mtakatifu wala kipawa cha lugha.
B. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa "ahadi", siyo amri.
C. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulifuatana na miujiza na upuzio.
D. Ubatizo wa Roho Mtakatifu haukukusudia ondoleo la dhambi wala kumweka mtu katika Kristo.

III. KORNELIO NA NYUMBA YAKE WALIBATIZWA KATIKA ROHO MTAKATIFU:
A. Kornelio "alibatizwa katika Roho Mtakatifu", Mdo. 11:15-16.
B. Hii iliitwa "karama ile ile", Mdo. 11:17, lakini hii ilikuwa tofauti na yote, isipokuwa yaliyotokea "mwanzo", 11:15, na juu "yetu" (yaani "Mitume tu.").

Maangalizi :

Ni wazi kwamba hiyo "karama ile ile "haikuwa kile "kipawa cha Roho
Mtakatifu" ambacho waamini wote wameahidiwa; kama ingekuwa hivyo, Je ingaliandikwa kwa urefu wa namna ile?

C. Ubatizo wa Kornelio katika Roho Mtakatifu ulitangulia wongofu wake, kwa hiyo ulikuwa kabla hajapokea ondoleo la dhambi, Mdo. 10:44. Sasa soma Mdo.
11:4, "kwa taratibu," 11:15, Roho Mtakatifu alitangulia kabla ya imani, toba au ubatizo! Lakini "kipawa cha Roho Mtakatifu" hufuata baada ya ubatizo kwa ondoleo la dhambi.

Maangalizi:



1. Kupokelewa kwa Roho Mtakatifu juu ya nyumba ya Kornelio hakukuonyesha kwamba yeye amekwisha kuwa mtoto wa Mungu.
2. Neno lile "kipawa" linaweza kuwa na maana mbalimbali tofauti kufuatana na mistari iliyopo. Mfano: Gal. 1:1 na Fil. 2:25 (Mitume). Katika mstari wa kwanza, ni mmoja wa wale kumi na wawili; katika mstari wa pili, ni "mmoja aliyetumwa na usharika".
D. Baada ya kupokea ile karama ya mwujiza ya Roho Mtakatifu, Kornelio na nyumba yake waIiagizwa wabatizwe, Mdo. 10:48; kwa ondoleo la dhahmbi, Mdo.
2:38; wapokee kipawa cha Roho Mtakatifu, Mdo. 2:38-39.
E. Kwa nini nyumba ya Kornelio waliupokea Ubatizo wa Roho Mtakatifu?
1. IIi ionyeshwe kwamba Mungu alikuwa amepokea, mataifa vile vile na
Wayahudi, Mdo. 11:17-18.
2. IIi kanisa la Kristo liunganishwe, Mdo. 11:19-26. Maangalizi:
Mungu alikuwa akingoja kwa muda wa miaka kama kumi, mpaka aliwaita watu wake kuwa Wakristo. Alifanya .hivyo tu, baada Wayahudi walikuwa wameyatambua mataifa kuwa warithi wa uzima pamoja nao, na baada Wayahudi na mataifa walikuwa wakisali pamoja katika usharika mmoja.

AZIMIO:

Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa maonyesho ya Mungu ya kushangaza na yenye mwujiza! Ulikuwa mwanzo wa wakati mmoja maalum katika Ufalme wa Mungu, na kwa hiyo ndio wenye maana kwa watu wa Mungu. Matokeo yake yanaonekana hata leo,
lakini hakuna mtu leo awezaye kujinenakuwa na uwezo, mathibitisho, na maonyesho ya aina hii. Lakini mtoto wa Mungu mpaka leo hupata kipawa cha "kuenea pote" cha Roho Mtakatifu.


KIPAWA CHA KUENEA POTE CHA ROHO MTAKATIFU

INGIZO:

A. "Kipawa cha Roho Mtakatifu" ni Roho Mtakatifu mwenyewe anayetolewa kwa kila mtu a1iyebatizwa akiwa mwamini atubuye.
B. Kuonyesha kwamba kipawa cha Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu mwenyewe, tena ni kipawa cha kuenea pote kwa watoto wa Mungu.
C. Roho Mtakatifu ameahidiwa kwa njia ya lIpuzio kwa watoto wote wa Mungu; kwa hiyo aweza kuitwa "kipawa cha kuenea pote".

I. "KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU" KATIKA Mdo. 2:38 NI NINI?
A. "Kipawa ndicho Roho Mtakatifu (jinsi ya kujulisha mwenyewe)" A. T. Robertson, Word Pictures of Greek New Testament.
B. "Jinsi ya kujulisha kitu", N. Turner, Grammar of New Testament Greek. Kipawa kilikuwa Roho Mtakatifu.
C. Mara nyingi Mungu hayasemi yale ambayo "mimi" nataka ayaseme, lakini hata hivyo nina wajibu wa kujifunza na kuyapokea yale aliyoyasema.

II. AHADI ILIKUWA YA KUENEA POTE:
A."Ahadi ni kwa ajili ya Wayahudi, na kwa watoto wao, na kwa wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Mungu." Mdo. 2:39. Kwa hiyo, kwa ajili ya Wayahudi na mataifa - kwa watu wote, ling. Efe. 2:11-13 (na mengine).
B. Wote "walioitwa". Mungu aitaje? Mdo. 2:37 "wakachomwa mioyo yao, Mdo.
2:38 wafanye nini, Mdo. 2:40 wamc:onywa kufanya hivyo, Mdo. 2:41 waliolipokea neno lake wakabatizwa, Mdo. 2:47 "wakiokolewa"; kwa hiyo wote walioyapokea masharti, wameahidiwa Roho. Wakati wote wanadamu waweza kusikia injili na kuitii, Mungu ataitimiza ahadi yake ya kipawa cha Roho Mtakatifu.

III. WOKOVU - JE, HUO NDIO KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU?
A. SIYO! Hakusema, "tubuni mkabatizwe kwa ondoleo la dhambi mtaokolewa." Wokovu limo ndani ya ondoleo la dhambi. Ni lingine lililoahidiwa. Ni nini?
B. Roho Mtakatifu mwenyewe!

IV. NENO - JE, HILO NDILO KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU?
SIYO! Sababu "neno" halie1ezwi hivyo. Walilipokea neno kabla hawajabatizwa, kwa sababu walikuwa "wamekatwa". "Maneno" yaliwaambia wafanye nini. Wote walioyatenda walilipokea. "neno"; hata hivyo bade kitu kingine kilielezwa. Neno na roho siyo kitu kimoja. "Kipawa" kilikuwa kimeahidiwa, wakati waliokuwa wamekwisha pokea neno na kubatizwa; kwa hiyo kile' "kipawa" siyo "neno la Mungu .. " Efe. 6:17.

V. MISTARI MINGINE IHUSUYO WAKRISTO WAKIPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU:


A. Mdo. 5:32, mstari huu wasema kwamba Roho Mtakatifu hutolewa kwa wale watiio. Roho Mtalcatifu alikuwa ameahidiwa kwa wale waitiio injili, Mdo. 2:38. Watiio watajwa katika mistari yote miwili; jinsi gani twaweza lcuepuka, tusidhani kwamba Roho Mtalcatifu mwenyewe ametajwa katika mistari hiyo miwili?
B. Mdo. 6:3, watu hawa walikuwa "wenye kujawa na Roho Mtakatifu". Bila shaka, hao ndio wale wale wa Mdo. 2:38 na 5:32. Lakini, hata kama ikawa hivyo walikuwa tofauti na wale wanafunzi wengine kwa aina fulani.

Sababu wote walikuwa na kile kipawa, bila shaka walikuwa wamejitolea maisha yao kwa Roho na kwa Mungu, zidi kuliko wengine walifanya. Miujiza haihusiki wala haitajwi hapo.
C. Rum. 8, Roho, Roho wa Mungu, na Roho wa Kristo hukaa ndani ya Wakristo, Rum. 8:9. Katika 8:11, neno lile "kukaa" latoka kwa neno "nyumba au makao". Neno hila halihusiki na mahali pa kusimamia kwa mud a tu, bali lahusika na mahali pa kuishia kwa kudumu. Lahusika na kukaa kwa kudumu. Roho Mtakatifu siyo mgeni wa siku moja tu, bali ni mkazi wa kudumu.
1. "Anakaa" ndani yako hasa. Nini inayoufanya mstari huo kuwa kama mfano?
2. Hautaji wala hauhusiki na mfano wa kitu kingine.  "Kila neno linenwalo, lazima lifahamike kufuatana na maana yake ya kawaida, isipokuwa jambo Ienyewe linenwalo au maneno mengine yanayotangulia na kufuata yanaikataza kwa jinsi maalum. Sheria hii yahusu maneno yote, tena ni sheria iliyo lazima." J. D. Bales, The Holy Spirit and Christians, uk. 10.
D. Gal. 4:4-6, siyo kwa maoni yetu wala Kwa upuzio, bali ni kwa Roho kwamba twalia, "Aba, yaani, Baba"" Roho yupi anakaa ndani yetu? Kwa hiyo tunaye shahidi (Rum. 8:16) pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.
E. 1 Kor. 6:19-20, Paulo adhihirisha, kwa nini Wakristo wasitende uasherati. Paulo asema juu ya mwili wa mwanadamu uonekanao. Mwili huo ndio hekalu la Mungu, ambalo Mungu anakaa ndani yake kwa Roho Mtakatifu. Asema wazi juu ya "Roho aliye ndani yenu". Labda hiyo ndiyo sababu kwamba kanisa au mwili wa Kristo huitwa hekalu la Roho Mtakatifu, 1 Kor. 3:16.

Maangalizi:

1. Mistari hii yaonyesha wazi kabisa kwamba Roho Mtakatifu akaa ndani ya watu wa Mungu.
2. Anakaa ndani ya mtu zaidi ya mmoja, wakati ule ule.
3. Tena hakuna lolote lililo kinyume cha akili, uwezekano, au maandiko, kuhusu kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani ya mwili wa kibinadamu.

VI. ROHO MTAKATIFU AKIKAA "NDANI YA NENO TU":
A. Kuna ndugu wanyofu wengi wenye akili waammlO kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya Wakristo kwa njia ya neno tu. Lakini sisi hatuamini hayo. Ndugu hao waingia matatizo magumu ambayo hawawezi kuyashinda kwa akili wala kwa maandiko.


1. Hakuna mstari hata mmoja usemao kwamba hivyo ndivyo Roho
Mtakatifu akaavyo ndani yetu.
2. Hakuna mstari hata mmoja usemao kwamba Kristo na Mungu wakaa ndani yetu kwa njia ya neno tu, Efe. 2:22.
3. Kupokelewa kwa Roho Mtakatifu (ahadi yake katika Mdo. 2:38)
kulikuwa baada ya kulisikia na kulitii neno.
4. Tumetiwa muhuri na Roho Mtakatifu katika Kristo, Efe. 1:13, lakini kwanza mmebatizwa katika Kristo, Gal. 3:27.
B. Kwa hiyo tumefahamu ya kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya Mkristo binafsi, na siyo kwa maneno ya Roho tu, wakati maneno hayo yakipokelewa.

VII. ROHO MTAKATIFU ATAKAA NDANI YA MKRISTO KWA MUDA GANI?
A. Lini na kwa sababu gani Roho Mtakatifu anamwacha mtoto wa Mungu? Swali hilo ni lile lile Ia kuuliza, Iini yule mtoto wa Mungu anaanguka katika neema asiirudie tena?
B. Kanisa la Korintho lilikuwa usharika uliokuwa na ukosefu wa dhambi nyingi; hata hivyo kanisa lilikuwa hekalu la Roho Mtakatifu, 1 Kor. 3:16; na washarika hawakuwa mali yao wenyewe, maana "Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu". 1
Kor. 6:19.
C. Roho Mtakatifu hatafuti udhuru wa kutuacha, bali anahamu kubwa ya kuwa msaidizi wetu. Hata hivyo kuanguka kabisa huweza kutokea, na hutokea mara nyingi, Ebr. 6:6; 10:26-31. Mkristo aweza kujifanya moyo wake mgumu kiasi hiki asiweze kumrudia Mungu tena. Wajibu wetu ni wazi. Kuishi maisha yetu kwa
ajili ya Mungu.
D. Wakati wote ambao tunajaribu na kuendelea mbe1e zaidi, tusiogope. Roho hatatuacha; lakini mara moja akituacha, tutakuwa tumekufa kiroho mile1e. Yakobo aliyaeleza hayo kwa mfano wa kimwili, ili afundishe somo la kiroho. "Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa." Yak. 2:26.

AZIMIO:

Kati ya faida na wajibu ambazo Mkristo anazifurahia, kipawa cha Roho Mtakatifu ndicho cha muhimu sana. lIe ahadi iliyotolewa na watu waliotiwa pumzi ya Mungu wakati wa mahubiri ya kwanza ya injili, yaonyesha jinsi Mungu aonavyo juu ya Roho akikaa ndani ya Mkristo. Mungu atusaidie tuweke hazina ya jambo hila ili tujitahidi kuishi maisha yetu kufuatana na hayo.

No comments:

Post a Comment