Saturday 31 December 2016

Mafundisho Ya Msingi Wa Kikristo

MUNGU - KUWAKO KWAKE NA HALl YAKE

INGIZO:

A. Imani ya mwanadamu iliyo ya zamani kabisa na iliyo ya maana kubwa mno ni imani yake kwa Mungu. Bila ya imani ya aina hiyo maisha ya mwanadamu hayastahili kuwako, yaani hayana maana. Lakini ufahamu wa kweli unahitajika vile vile.

B. Nia yake mwanadamu juu ya Mungu hudhihirisha kadiri na aina ya ibada na utumishi wake. Ni kama kutufinyanga kweli maisha na matendo yetu. Mwanadamu ni matokeo ya imani yake.

C. Kusudi la masomo hayo ni kukupangia imani kwa Mungu iendayo ndani zaidi, na kukupa ufahamu wa Mungu ulio saw a na wa kukuwezesha kuishi kwa ajili yake na kukataa imani juu yake yenye ukosefu.

I. JINA LA "MUNGU".
A. Neno hila "Mungu" latokea mara 4067 katika Biblia. B. Mungu alikuwako kabla ya Biblia. Mwa. 1:1, Yn. 1:8.
C. Kuwa kwake kwa milele, kuwako kwake, na kuwapo kwake huhakikishwa katika Biblia.
D. Ni "mpumbavu" tu asemaye kwamba hakuna Mungu, Zab. 14:1.
1. Nyakati zote watu fulani walijaribu kumkanusha Mungu. Lakini walimthibitisha tu.
2. Katika mji wa Oxford, nchi ya Uingereza, mtu fulani aliwahutubia wasikilizaji wengi akisema, Nitathibitisha kwamba hakuna Mungu nikimbisha mpaka ataniua; akasema, "Hakuna Mungu". Msikilizaji mmoja aliyekaa nyuma akamwambia, "Namna' gani, wewe uduvi mdogo, Mungu hatapoteza mud a wake akimwua uduvi mdogo kama wewe."
E. Majina ya Mungu.
1. Jina liitwalo "Elohim" - Mara nyingine hutumika pamoja na "definite article", mara nyingine bila yake. Hutokea mara 2555 katika A.K.; mara
2310 kati yake hutaja Mungu yule mmoja wa pekee kwenye uhai, lakini mara 245 hutumika kwa njia nyingine isiyo ya maana kubwa kama ile. Labda "Elohim" alikuwa kama "Yule Mmoja wa, pekee aliyejifunua mbele ya mwanadamu kama mwumbaji, mtawala na Bwana". Lilikuwa jina lake la kipekee ambalo lisitumike kwa mwingine. "Mungu (EMhim, katika wingi) aliziumba (kat. umoja) mbingu na nchi."

Shetani aliingiza uzushi wa kwanza, Mwa. 3:5, alipowaeleza wengine watajulikana kwa jina hilo. Ibada ya Elohim ilikuwal imechafuka, watu wakitaja cho chote kwa jina hilo. Mwa. 35:1, 24. Hapa Elohim lilikuwa kama hirizi au sanamu. Mwa. 31:19 (toraphim) mst. 30 Elohim. Kut.
12:12; Law. 19:4; Kut. 32:3-5. Yatofautishwa kati ya Jehovah na Elohim


zote, Kut. 18:1l; Kut. 20:3; 23:13; Kum. 4:39. Bwana alijitahidi kuwafundisha Waisraeli kwamba jina la Elohim ni jina lake peke yake.

2. Jina la Elohim na Utatu. Elohim, likiwa neno katika wingi, hairidhii wingi wa miungu (polytheism); lakini yatupasa tuufikirie uwezekano wa wingi katika Uungu; Mwa. 1:26. Rapo neno katika wingi latumika, ikiwa Mwa. 1:1 neno katika umoja Iaonekana. Waebrainia walipendelea kutoa maneno yaliyo katika hali ya wingi ili kwa maneno hayo maana maalum na ya mtindo ionekane; ling. Damu, Maji, Hekima, Wokovu, Maisha, n.k. Yaani hali{ya umoja ya maneno hayo haikutosha kueleza yote ambayo mwandishi aliyakusudia. Majina mengine ya Mungu ni katika hali ya wingi, Mhu. 12:1 (Waumbaji, kat. wingi).

3. Matumizi mengine ya jina hilo "Elohim" Kut. 4:16, hapo maana yake ni kuwa mjumbe wake, siyo kuwa sawa naye, ling. Zek. 12:8. Hapo jina la Mungu lilitumika kwa mtu aliyekuwa mjumbe wake, Kut. 7:1. Hayo yalielezwa wazi na Yesu katika Yn. 10:34-36 (Zab. 82; Kut. 22:8-9).
Kama wale walikuwa wajumbe wa Mungu, Yesu alikuwa mjumbe wake zaidi. Mara nyingine waamuzi walikuwa wametajwa Elohim, Kut. 21:6. Hapo maana yake siyo kwamba watu watajwao Elohim wastahili kuabudiwa, bali watu hao ni jamii ya mahakimu watajwao jina hila kwa sababu watenda kazi badala ya yu1e Elohim mmoja na wa kweli, 19:17.

4. Utumiaji wa jina la Elohim kwa malaika. Zab. 8, "Malaika kwa
Kiebrania ni Elohim".

5. Mwenyezi - Shaddai. Jina hilo kwa kweli humkumbusha msomaji
Mwebrania utajiri na neema ya Mungu. Mpaji wa kila kitu, Mwa. 35:11;
43:14; Mwa. 49:25 (Ezi ya Mungu ya El - Shaddi - Uzuri wake).

6. Bwana - Adonai - Jina hilo limetoka kwa neno lile Adon ambalo maana yake ni Mungu, au kwa lugha ya Kiyunani ni Kyrios - Bwana; ling. Mwa.
43:24; Mwa. 24:9. Jina hila laweka wazi ukweli ule kwamba kila mwanachama wa jamii nzima ya kibinadamu ni mali ya Mungu, na kwa hiyo Mungu anataka utii kamili wa wote. Jina hilo lilitumika mara ya kwanza kwa Mungu katika Mwa. 15:2; 15:8; 18:3. Mwa. 15:2 yasemwa hasa, "Bwana wangu Jehovah". Kum. 10:17 "Bwana wa Mabwana", au hasa, "Mkuu wa Wakuu", m.y. Mungu Mkuu wa wote walio na mamlaka ya kuyashika mikononi mwao. Jinsi matakwa ya Mungu kwa utumishi wa mwanadamu yaonekanavyokwa jina hila Adoni, yajulikana katika Mal.
1:6.

7. Aliye Juu - Elion - Jina hilo lilitumika mara ya kwanza katika Mwa.
14:18-22, Hes. 24:16; Kum. 32:8; Mdo. 17:26. Katika Zab. 89:27, jina hilo latumika kwa Masihi. Neno hila halitokei katika matumizi ya lugha ya dini tu, ling. Mwa. 40: 17; 1 Fa!. 9: 8; Neh. 3:25, n.k.



8. Jehovah. Jina hila latokea mara 5,500 katika A.KMara nyingi neno lile "Bwana" limeandikwa badala yake. Katika tafsiri nyingi za lugha nyingine "Jehovah" hutafsiriwa kwa "Aliye wa milele". Kama neno
laweza kujulisha wazi maana yake nini, ni neno hilo. Yafahamika kwamba
Jehovah ni jil1a la binafsi ambalo hutumika kwa Mungu, yaani kwa Mungu tu. Fikirie Kut. 3:14; 6:1-3, "Mistari hii miwili ikitazamiwa pamoja yafafanua mambo hayo yafuatayo:

Kwanza, hata kama jina la Jehovah lilitumika sana kama jina la Elohim wa Mababa Wakuu wa A.K., hat a hivyo maana yake iliyo kamili haikufunuliwa mbele yao; Pili, jina hila lilihusika hasa na utimilizo wa agano na ahadi ya Mungu ili sasa baada ya kame nyingi zilizopita maana ya kweli ya jina hilo iwekwe wazi kwa ufunuo wa Yule binafsi mwenye uhai, akifanya kazi kwa ajili ya Waisraeli ili ahadi ile iliyofanyika kwa
Mababa itimizwe. Hivyo ndivyo, fikra ile adhimu juu ya Mungu wa milele asiyebadilika akikaa kuwa mwaminifu katika neno lake kwa muda wa vizazi vingi, ilivyoanza kufahamika katika mawazo ya Waisraeli, na yale yaliyotumainiwa na kutiwa muhuri wa jina hila nyakati za Mababa
Wakuu, yalianza kujifunua yenyewe kuwa katika hali ya ukweli. Kuwako kwa Mungu binafsi, jinsi aendeleavyo kufanya kazi pamoja na wanadamu, jinsi ahadi zake zisivyobadilika, na ufunuo kamili wa neema yake ikomboayo, hayo yote yakusanyika katika jina hilo Jehovah. Siyo "Elohim asema hivi", bali ndiyo "Jehovah asema hivi", ambalo ndilo ingizo 1a kawaida 1a taarifa za manabii. Akiwa Jehovah, ndiyo Mungu amekuwa Mwokozi wa Waisraeli, na kama Jehovah akomboa u1imwengu; na huo ndio ukweli uliowekwa ndani ya jina la Yesu, ambalo maana yake ndiyo JehovahMwokozi hasa."

Katika Mwa. 9:26 Jehovah ni MUl1gu wa Shemu; Mwa. 14:22 yadhaniwa kuwa sawa na E1-Elion "Mungu aliye Juu". Katika Mwa. 15:1 "neno la Jehovah -----" Jehovah mwenyewe hasa. Aliye mhukumu, Mwa. 18:25. Mababa Wakuu walishauriana na Jehovah, Mwa. 18:1-2; 28:13-17; 32:24. Musa alizungumza naye uso kwa uso, Kut. 33:9-11. Ufunuo ulifanyika na Jehovah, Kut. 34:6-7. "Hapo twaona maana kamili ya Jehovah - neema yake na nafsi yake ya hukumu; yaani kama jina la Elohim huweka wazi nguvu ya Mungu aliye mwumbaji na mfululizaji, Jina la Shaddai likionyesha uzuri wake, na jina hilo la Jehovah ambalo hufunua tabia zake maalum zisizogeuka, yaani tabia zake za neema na hukumu, akionekana kuwa Baba, Rafiki na Mtawala mwenye adili.

9. Bwana wa majeshi (jina "Jehovah" 1atumiwa) au Bwana wa Sabbato, jina lile 1a kwanza likiwa utafsiri wa lile la pili. 1 Sam. 1:3, Rum. 9:29; Yak. 5:4 na vv. Kut. 12:41; Waisrae1i ni "majeshi ya Bwana", maana yake kwamba Jehovah ni akida au mlinzi wao. Wengine hutaja "Mwenye mbingu". Labda Myahudi aliifahamu maana yake hivi kwamba Mungu


ana vyama vyote vya ulimwengu na vya dhamira chin'i ya mam1aka na madaraka yake akivisimamia jinsi atakavyo. Taz. Zab. 147:4; Isa. 40:26.

10. Malaika wa Bwana, jina la Jehovah latumika tena. Mwa. 32:1-3; "Malaika afahamika kuwa Jehovah mwenyewe. Mwa. 16:7-13; Zek. 3:2, "Malaika wa Bwana, - Bwana na akukemee". Wengine waona kwamba ni Kristo; lakini hakuna hakika; taz. Mt. 2:13. Katika Zek. 1:12 Jehovah na Malaika ni tofauti, kwa sababu Malaika amsihi Jehovah. Malaika yule ali- kuwa wakili wake Jehovah akiyaimarisha na kuyatimiliza mapenzi ya Jehovah.

II. USHUHUDA WA KUWAKO KWA MUNGU

A.  Ushuhuda wa Kihistoria: Kuwako kwake kwa kihistoria hakuna mashaka.
1. Mungu alimwumba mwanadamu. (Kama mwanadamu alimwumba
Mungu, ni nani aliyemwumba mwanadamu?)
2. Katika fikra za mwanadamu kutoka zamani sana ni imani yake kwa
Kitu maalum cha Juu.
3. "Hata taifa ambalo hali yake ni ya kishenzi kabisa, na hata watu wale wasiostaarabika, hata wao wamwamini Mungu,” alisema Cicero.
4. Shuhuda za kihistoria zimekuwa za dunia nzima kutoka mwanzo wa wakati na wa mwanadamu.
B. Ushuhuda zihusuzo ulimwengu ulivyo (cosmological evidence):
1. Kutoka mwanzo wa wakati wanadamu walikuwa wameishi katika ulimwengu mzuri mno wenye utaratibu.
2. Juu ya uzuri wa ulimwengu ambao mwanadamu huishi ndani yake, mmoja alisema, "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake." (Zab. 19:1).
3. Mbingu na dunia hazikuwa zimetokea kwa bahati, 2 Pet. 3:5.
4. Hapa duniani twapata ushuhuda jinsi Mungu alivyoumba kwa mikono yake.
a. Paulo alisema, "Kwa sababu mambo yake yasivyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, ... " Rum. 1:20.
b. Moyo wa mwanadamu huona mambo ambayo akili yake haiwezi kuyaona.
c. Mwasi mmoja wa Kifaransa aliwaambia wakulima fulani, "Nitaubomoa mnara wa kanisa lenu ili msiwe na kitu cha kuwakumbusha imani yenu ya usihiri tena." Wakulima wakajibu, "Huwezi kubomoa nyota".
C. Ushuhuda unaomgusa mwanadamu ndani ya moyo wake (intuitive):
1. "Mwanadamu alikuwa am eon a kwa moyo wake kwanza, kabla hajaanza kufikiri kwa akili yake."
2. Kisa juu ya bata Bukini wawili wa shamba huko Amerika ya Kusini. Wakati wa uhamaji hao wawili walifanya ya ajabu. Yule dumeakiwa mbele akienda moja kwa moja, yule jike alikwenda kuelekea kusini ya mashariki. Yule dume alianza kuruka na kumwita yule jike kwa wito wa


kumsihi sana. Baada ya muda mfupi tu dume aliona kwamba yule jike alikuwa, amevunja ubawa wake. Lakini hata hivyo dume hakumwacha. Hali hii ya kusihi ni kitu cha msingi ndani ya mwanadaamu.
3. Ushuhuda unaomgusa mwanadamu ndani ya moyo wake si njozi iliyo tupu, bali ni kitu muhimu kweli.
4. Augustino alisema, "Mioyo yetu haiwezi kupata raha mpaka itapumzika ndani ya Mungu."
5. Siku fulani kijana mmoja alikuwa amerusha tiara yake. Mtu mmoja akamjia akamwuliza afallyaje? Yule kijana akajibu, "Ninarusha tiara yangu." Yule mtu akasema, "Siwezi kuiona". Kijana huyo akajibu, 'Hata mimi siwezi kuiona, lakini najua kwamba ipo sababu inavuta."
D. Ushuhuda wa mambo tupatayo kuyafahamu kwa njia ya kidini:
1. Kama wale waliofariki tangu wakati wa Kaini wangeweza kufufuka na kusema, tungepata kufaharnu kutoka kwao kwarnba Mungu yupo.
2. Twajua kutoka kwa mambo mbalimbali ya maisha yetu kwamba Mungu wa ulimwengu huu yupo.
3. Labda mwingine ana ujuzi mkubwa zaidi katika mambo ya saiansi n.k. kuliko sisi, na kutoka kwa ujuzi wake 1abda atajaribu kutoa hoja kwamba hakuna Mungu. Lakini "futi sita za udongo zafanya watu wote kuwa sawa"; mfuasi wa Mungu ana mbingu, wa1akini yule asiyemwamini Mungu, ana jehanum.
E. Ushuhuda wa Biblia.


III. TABlA ZA MUNGU - HALl YAKE
A. Utawala na nguvu zote (Omnipotence) za Mungu.
1. Mungu aliumba kila kitu kwa neno la nguvu yake.  Alisema, na vitu vyote vilikuwa 'vimetokea (Uumbaji). Mwa, 1:3.
2. Paulo alisema, "Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu," Ebr. 11 :3.
3. Mungu ana uwezo kuharibu roho na mwili katika Jehanum. Mt. 10:28.
4. Kwa nguvu yake Mungu kuta za Yeriko, zilibomolewa, jua lilikuwa limesimama, waliofariki walikuwa wamefufuliwa, viwete waliponywa, viziwi walifumbuliwa masikio yao, kaburi Yesu lilifunguliwa, na Kristo alikuwa amefufuka.
5. Kwa nini mti mwingine huzaa matunda merna na mwingine huzaa matunda yenye sumu? Kwa nini wanyama wengine huonekana kuwa na akili zaidi kuliko wengine? Kwa nini mimea mii1gine huzaa matunda mara nyingi ki1a mwaka na mingine huzaa mara moja tu kwa mwaka? Jibu la pekee kwa maswali hayo ni Utawala wa Murigu katika yote. Zab.
135:6.
6. "Kama Mungu ana nguvu zote, kwa nini basi kuna vita, maovu n.k.?", swali hilo huulizwa na watu wengi.
a. Jibu kwa swali hila lapatikana Yn. 18:36, "Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, Mt. 6:10, "Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. "


b. Lk. 2, Malaika hawakuwatangazia Makuhani Wakuu habari za Kuzaliwa kwa Yesu, ingawa wale walikuwa viongozi wa dini wa sikuzile. Hata hivyo malaika waliwaendea wachungaji tu waliokaa peke yao.
c. Mara nyingi Mungu hayatimizi mambo kwa jinsi ile wanadamu watakavyo ayatimize; Lakini hata hivyo Mungu ana nguvu zote.
d. Amani ni kitu cha binafsi. Imo mioyoni mwa wale wafanyao mapenzi ya Mungu.
e. Kaisari Napoleoni Bonaparte alikuwa amemwaga damu za watu wengi katika nchi nyirtgi akijaribu kushika ufalme wake kwa nguvu. Kabla hajafa akikaa katika kisiwa cha St. Helena, aliungama kwamba upo ufalme mmoja tu udumuo milele yaani ufalme wa Kristo uliokuwa umeanzishwa na kudurnishwa kwa upendo.
B. Kujua yote (Omniscience) na Hekima ya Mungu:
1. Mungu alijua kila kitu kabla ya wakati, ataendelea kujua yote baada ya wakati.
2. Kila kituni wazi na tupu mbele ya Mungu. Ebr. 4:13.
3. Paulo alieleza hekima ya Mungu katika 1 Kor. l:20-25.
4. Kuanzia na mwanamke yule wa kwanza Hawa mpaka siku hizi, wanadamu wamejiona wenyewe kuwa na hekima kubwa zaidi kuliko Mungu, lakini baadaye wameonekana kuwa wapumbavu.
5. Isa. 55:8-9, Ukijumlisha hekima zote za watu wote wenye ujuzi, utapata kastabini tu ya hekima ile aliyo nayo Mungu.
C. Kuwako kwa Mungu mahali po pote (Omnipresence):
1. Mungu yupo ndani ya ulimwcngu huu na nje ya ulimwengu huu vilevile. Utukufu wake upo po pate.
2. Mungu yupo pamoja na wale wanaoona uchungu hapa na po pote. Yupo nchini pa wale waliofariki hapa na po pote. Yupo pamoja na wale
wahubiri na wamissionari wengi - nchini hapa na katika dunia nzima.
3. Mungu hayupo po pote katika maisha hayo tu, bali yeye ndiye peke yake vilevile ambaye anaweza kwenda pamoja na wapendwa wetu "kati ya bonde la uvuli wa mauti," Zab. 23:4.
4. Habari za mume na mkewe walioishi pamoja kwa muda wa miaka hamsini. Hawakutengana katika maisha yao hata kidogo. Wakati yule mke alipokuwa karibu na kufa, alimwambia mumewe, "Jim, mimi nipo karibu na bonde la mauti. Nenda pamoja nami." Akamshika mkono wake kwa nguvu kubwa zaidi kidogo. Yule mume akamjibu, "Mary, ningependa kwenda pamoja nawe, lakini ni Kristo peke yake ambaye anaweza kwenda pamoja nawe sasa". Hiyo ndiyo maana ya Kuwako kwa Mungu mahali po pote.

IV. MAFUNDISHO JUU YA MUNGU NA HALl YAKE YASIYO KWELI


Tangazo: Katika masomo mafupi kama hayo hatuwezi kueleza lo lote kwa urefu, lakini twawezakuorodhesha makosa machache yatokeayo tena na tena katika Dini mbalimbali zilizo ulimwenguni.

A. Dini ya Umormoni (Mormonism): Joseph Smith alikuwa amefundisha wingi wa miungu mbalimbali. Tangu mwaka 1844, Joseph Smith alikuwa akidharau kabisa mafundisho ya Kitabu cha Mormoni, yaani alieleza kwamba Mungu ni mwanadamu tualiyeinuliwa juu, na hata wanadamu waweza kuwa kama miungu.

Angalia:

1. "Kwanza, Mungu mwenyewe akaaye akitawazwa huko mbinguni ni mwanadamu kama mmojawenu, hii ndiyo siri iliyo kuu .... Mungu mwenyewe ambaye ni baba wa sisi sote alikuwa amekaa duniani kama Yesu Kristo mwenyewe alivyofanya .... Ni lazima mjifunze kuwa kama miungu wenyewe. Hakuna mtu awezaye kuwafundisha ninyi zaidi kuliko mimi niliwaeleza". (Times and Seasons, Kit. 5, uk. 613-614). Mtume wa Kimormoni, Orson Pratt, alitoa fundisho hilo lifuatalo juu ya wingi wa Miungu.
2. "Hiyo ndiyo ielezayo siri. Kama tungeshika millioni moja ya dunia mbalimbali kama dunia hii, na kama tungcjumlisha vipande vyao vyote, basi tungeona kwamba katika dunia hizo kuna miungu mingi zaidi kuliko vipande vile" (Journal of Discourses, Kit 2, uk. 345).
3. Kanisa la Kimormoni lafundisha kwamba Mungu mwenyewe alikuwa na baba yake, na baba huyo alikuwa na baba vilevile, n.k. (Ni kama kusema kwamba wewe u babu yako mwenyewe!! A. M. C.) Brigam Young alisema, "Ndugu Kimbell alipasha usemi wa Nabii Yosefu kwamba asingemwabudu Mungu yule ambayc hanababa; na mimi sijui
kwamba angefanya hivyo kama asingekuwa na mama; neno lile moja ni la upuzi kama lile lingine" (Journal of Discourses, Kit. 9, uk. 286).
4. Herbert C. Kimbell aliyekuwa mmojawao Wakuu wa Wakati wa
Kwanza, alisema " ... halafu tutamrudia Baba yetu yaani Mungu
aliyekuwa ameunganishwa na mmoja ambaye alikuwa amekaa kabla yake; na baba huyo alikuwa ameunganishwa na mmoja vilevile ambaye alikuwa amekaa kabla yake tena,na kadhalika", (Journal of Discourses, Kit. 5, uk.
19), n.k. Ad-Nauseam! (= mpaka kupuzia).
B. Dini ya Uhindi - "Kuna Kitu kimoja cha asili chenye ukweli, ambacho ni cha juu kuliko vyote, kisichochanganyika na kitu kingine, ambacho kinaitwa Brahman. Brahman ni kama utulivu. Hakuna maneno yawezayo . kuueleza; hakuna wazo ila kibinadainu ·liwezalo kuchungua tabia yake; hakuna filosofia iwezayo kueleza maana yake.Ni zaidi na nje ya yote yaliyowekwa chini ya nguvu
ya mauti na maisha. Ni zaidi ya ufahamu wa yule ajuaye na yale y:mayofahamika. Ni zaidi kuliko maelezo yote yanayoelezwa kuwa yakupendeza au ya kutokupe- ndeza katika maisha yetu yenye mwisho wake. Maana yake haina mwisho. Haiwezi kushikwa ndani ya mipaka yo yote. Kutokana na hayo ni ile Halisi hasa isiyohusika na ulimwengu huu, tena isiyowekwa chini ya vitendo vyo vyote


walachini ya matokeo yake. Kwa hiyo tabia kamili ya ile Brahman haiwezi kujulikana wazi, lakini hata hivi ni yule "Mimi' wa kweli." (Introducing Hindusm, na Malcolm Pitt, uk. 17-18).
C. Dini ya Uislamu - "Tendo lile moja kubwa kabisa la nabii Muhammed lilikuwa lile la kuanzisha dini ile ambayo inashika karibu kwa ushupavu kwamba Mungu
ni mmoja ... Nguvu yake na mamlaka yake juu ya viumbe vyote, hiyo ndiyo inayodhihirishwa mno katika Uislamu kiasi hiki kwamba ni vigumu kwa Mwislamu kumwita Mungu kuwa Mungu wa upendo au kumtaja Baba. Utakatifu na haki yake Mungu hazidhihirishwi kuwa msingi wa matendo yote, kama zilivyo katika Agano la Kale. Allah ajulikana kuwa 'Bwana wa dunia zote, au 'Mtawala wa ulimwengu' na kama 'Bwana wa Siku ya Hukumu' .... Kufuatana na mafundisho ya Kiislamu, nguvu na kutokubalika kwa Allah zamfanya kuwa mwumbaji wa vitu vyote, yaani wa vitu vyema na vitu vibaya vile vile; fundisho hilo huelezwa katika sehemu nyingi za Kurani.

"Kuna orodha ya majina mazuri tisini na tisa ya Mungu yanayojulikana kwa Waislamu. Yasemeka kwamba ni ngamia tu ajuaye jina lile la mia moja, na hiyo ndiyo inayompa ngamia tabia yake ya heshima. Tasbihi ya kawaida ya Kiislamu ina shanga tisini na tisa,au vifungu vitatu vya shanga thelathini na tatu; na kila ushanga umewekwa badala ya jina moja la yale 'majina mazuri' ya Allah.

"Dr. Paul Harrison ambaye ni mmissionari wa miaka mingi katika nchi ya Arabia asema kwamba hawajui watu wengine ambao wanamfikiri Mungu kuwa juu
kabisa kama Waislamu, hata hivyo imani hii haigusi sana adilifu ya maisha yao ya kawaida." (Alama zimewekwa na mwandishi A. M. C.) Introducing Islam, na J. Christy Wilson, uk. 19, 20, 21.

D. Dini ya Uanismi - Maelezo yake: "Pundisho liIe la zamani ipo nguvu fulani (Anima Mundi, nafsi ya ulimwengu) ambayo haina sura yenyewe, lakini haiwezi kutengwa na vitu, tena yatia vitu sura na mwendo wao; ni kama kutia roho au nafsi katika vitu visivyo na nafsi bado." Educational Book of Essential Knowledge, uk. 34.
1. Uanismi hupatikana sana katika dini zote za zamani,
lakini kwa kawaida Uanismi hupatikana hata katika dini zile maalum kama Ukristo, k.m. (viapo, dalili, ustahifu wa utajiri, nguzo zenye rangi, n.k. - Mkune Mwamerika, utapata mpagani vilevile!)
2. "Mwanismi kwa kawaida humwamini "Mungu mmoja aliye juu" - yaani Mungu ambaye kwa maneno afanana kidogo na Mungu wa Ukristo, lakini kwa vitendo nitofauti sana" Ingawa wafuasi wake wasema kwamba aliuumba ulimwengu, lakini mara nyingi haonekani kuwa na nguvu
nyingi. Yeye ni kama Mungu wa kwanza tu miongoni mwa miungu mingi ambayo ni sawa naye. Kwa kawaida ametengwa akikaa mbali na wanadamu, pia haabudiwi kwenye madhabahu yo yote wala haheshimiwi kwa kupewa zawadi zo zote." Introducing: Animism, na Eugene A. Nida, Will A. Smalley, uk. 15.


AZIMIO:

3. Katika Uanismi kuabudiwa kwa majadi kuna maana kubwa katika imani hii. Yanayohusu ufahamu, hofu na imani yao, mara nyingi ni vigumu sana kutofautisha kati ya ibada yao kwa majadi na ibada yao kwa miungu. Mungu kama Jehovah ni Mungu wa kigeni sana mbele yao ambaye hajulikani kwa wafuasi wa dini ile; lakini hata hivyo mara nyingi wapo tayari kujifunza jinsi ya kumtambua vema.
4. "Msingi mkubwa wa dini ya Uanismi ni hofu hasa.  Mwanismi huishi katika hofu kucha kutwa akiogopa pepo mbalimbali ambazo, kufuatana na imani yake, zamzunguka kila mahali. Ni zile pepo zilizo na madaraka na wajibu juu ya kila kitu kinachotokea. hakuna sababu nyingine za kawaida. Maisha yote katika kila jambo yamejaa hofu ya pepo. Nyakati zote kama zile za kuzaliwa kwa mtoto, arusi, kujenga nyumba, kupanda mimea au wakati wa mavuno, lazima pepo ziheshimiwe. Wanaoishi wanateswa na hofu kwa yule ambaye amekufa, wakifikiri kwamba pepo zake huzunguka kijiji chao kukisumbua. Sadaka hutolewa kwa njia ya madhabihu, ili pepo za yule aJiyefariki zitoke kwenda mahali pao. Hudhaniwa kwamba pepo hukaa kwenye mahali pa pekee, kama kwenye miamba ya mtindo, miti mitakatifu, maporomoko ya majiau chemchemi zenye maji yanayotumika kama dawa." Religions in a changing world, na Haward F. Vas, mtengenezaji, uk. 25.



Mtu mwaminifu hawezi kuwa na mashaka juu ya kuwako kwa Mungu. Kama akitoa mashaka ni kwa sababu amekataa ushuhuda uliopo po pote juu ya Mungu. Hali tukufu ya Mungu ni hivi kwamba Mungu aweza kufanya 10 late. Lakini tabia zake hazimruhusu Mungu kufanya zaidi kwa ajili ya mwanadamu kuliko amekwisha fanya. Hekima yake yamfanya Mungu alijue limfaalo mwanadamu zaidi, na kuwako kwake mahali po pote kwamwezesha kuwapo kila mahali wakati wo wote. Hivya ndivyo Mungu alivyopanga kila kitu vizuri. Kweli, Mungu ni Mungu Mkuu! Je, wataka kumtumikia?

No comments:

Post a Comment