INGIZO :
A. Vipawa vya mwujiza vya Roho
Mtakatifu vilitolewa na Mungu kwa
Mitume; viliweza
kugawanywa katika kanisa 1i1e la zamani kwa njia ya "Kuwekewa
mikono" ya Mitume; vilikoma wakati makundi hayo mawili yalipokufa na ufunuo wa maandiko ulipokuwa tayari.
B. Kuonyesha hali ya vipawa vya mwujiza; kuchunguza jinsi vilivyapoke1ewa na jinsi
vilivyogawanywa; kuonyesha vipawa vya mwujiza vilidumu kwa muda gani.
C. Katika masomo yetu mpaka sasa, tumeona ya kwamba "kipawa cha Roho Mtakatifu"
katika Mdo. 2:30 kilikuwa Roho Mtakatifu mwenyewe. Tuliona vile vile kwamba kili- kuwa ahadi ya kuenea po
pote kwa wote waaminio na kubatizwa wapate ondoleo la
dhambi. Tuliona kwamba Ubatizo wa Roha Mtakatifu uliwafikia Mitume tu,
isipokuwa
Kornelio na nyul11ba yake vile vile, ili ionyeshwe wazi kwal11ba Mungu amewapokea mataifa jinsi alivyowapokea Wayahudi. Mdo. 11:17-19. Sasa tutaingia somo juu
ya vipawa vya mwujiza vya Roha Mtakatifu, jinsi vitumikavya, jinsi vipatikanavyo, na jinsi
vikomavyo.
I. KULIKUWA NA "KIPAWA CHA MWUJIZA"
CHA ROHO MTAKATIFU:
A. Watu "waliowekewa mikono" ya Mitume walipokea
nguvu ya mwujiza. Mdo.
6:5-6, 8;
8:6-7, 13, 17-19; 19:1-7; Rum. 1:11.
B.
Lakini wale ambao Mitume "waliweka mikono" juu
yao, hawakuweza kuwagawanyia wengine kipawa hiki!
1.
Filipo alikuwa mtu wa
aina hii. Mdo. 6:5-6; Mdo.
8:7, 13.
2.
Mitume walihitajika wagawanye kipawa hiki. Mdo.
8:18.
3. Lakini hata Filipo alikuwa
na uweza akawabatiza, Mdo.
8:12-13; kwa hiyo walipokea
"kiwapa cha
Roha Mtakatifu" kama ilivyo Mdo.
2:38.
Maangalizi:
1.
Yaonekana ya kwamba "kipawa" katika Mdo.
2:38 hakikuwa cha mwujiza.
2.
Wale ambao Mitume waliweka
mikono juu yao, wakati walipoweza
kutenda miujiza, hawakuweza kuwagawanyia wengine hiki.
II.
KIPAWA HIKI CRA MWUJIZA KWA NJIA YA "KUWEKEWA MIKONO"
YA MITUME KWA WATU BINAFSI
FULANI.
A. Mitume "waliweka mikono" juu ya haa wafuatao:
1.
Wale Saba, Mdo. 6:5-6.
2.
Wale Wasamaria, Mdo. 8:
14-21.
3.
Wale Waefeso, Mdo.
19:1-7.
4.
Wale Warumi, Rum. 1:11, n.k.
B. Maonyesho ya mwujiza yalitokea.
1.
Kunena kwa lugha ya mwujiza yameorodheshwa, 1 Kor.
12:1; 12:4;
12:8-11;
I Kor. 12:28-31. (vipawa tisa vya mwujiza kwa
jumla).
Maangalizi:
1.
Roho Mtakatifu hakuto1ewa kwa kitendo ki1e
cha kuwekea mikono ya
Mitume, bali ilikuwa i1e
asili ya mwujiza tu iliyogawanyika.
2.
Hii haikuweza kupitishiwa kwa
ye yote mwingine.
3.
Miujiza ilishuhudiwa kila mara wakati Mitume walipogawanya kile kipawa cha mwujiza.
4.
Roho Mtakatifu kama kipawa alikuja kwa njia ya kuitii injili; Mdo.
2:38; maonyesho ya mwujiza yalitokea kwa
mikono ya Mitume tu.
III. KlLE " KIPAWA CHA MWUJIZA"
LAZIMA KIMEKOMA.
A. Kama kilitokea kwa mikono ya Mitume tu
basi
bila shaka haiwezekani kukitazamia siku hizi - kwa
hiyo siku hizi hakuna ushuhuda wa kweli wa miujiza ya Mitume na Kanisa
lile la zamani.
B.
Biblia yaonyesha jinsi miujiza ilivyotumika, Mk 16:16-20; Ebr.
2:1-4.
1.
Kuthibitisha neno
lao.
2.
Neno limekwisha thibitishwa.
3.
Kwa
hiyo hakuna haja
na miujiza siku
hizi.
Maangalizi:
Kwa njia hii, na
kwa njia hii tu, yawezekana kujua
kwamba msemaji alifundisha
ukweli.
C.
1 Kor. 13:8-12, mistari hii yafundisha wazi komo la mambo ya mwujiza:
1.
Unabii - lugha -
maarifa -
zote zitakoma. Hizo zilikuwa za mwujiza, 1
Kor. 14.
2.
Ijapo
ile
iliyo "kamili". Katika lugha ile ya asili ya Kiyunani, neno
lile
"kamili"
lipo katika mfano wa
kuonyesha kwamba ni kitu hasa, siyo mtu ..
3. Maelezo yaliyotolewa na
Paulo yaonyesha kwamba ile "kamili"
ndiyo ufunuo uliomalizika, mst. 12. Pia,
neno lile "kamili" lina maana ya kuwa "zima"
au "pevu".
Maangalizi:
1.
Kama ya Mwujiza yangewezekana au yangetokea leo, wateteaji wangevunja 1 Kor.
14 vibaya!
2.
Wakati kanisa lilipokuwa katika hali ya uchanga,
lilihitaji "misaada hii
ya pekee" '-
lakini hili siyo lazima siku
hizi. Ufunuo
uliomalizika
watukabidhi yote tunayohitaji, Yud. 1:3; 2 Pet.
1:3.
Swali :
Nini
inayohusu "mambo ya mwujiza"
yashuhudiwa katika dini siku hizi? AZIMIO:
Mungu alipowaumba mwanamume na mwanamke, hii ilikuwa imetokea kwa mwujiza;
baadaye sheria ya asili ilianza kazi.
Mungu alipoliunda kanisa liwepo, aliyatumia mambo ya mwujiza ili alianzishe na
kulisaidia kanisa katika uchanga
wake. Mwishowe
sheria iliyokuwa imefunuliwa ilianza
kazi: kwa hiyo madhumuni yetu ni ya kweli.
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
INGIZO :
A. Mungu alitenda miujiza akauweka Ubatizo wa mwujiza wa
Roho Mtakatifu. B. Kuonyesha Ubatizo wa mwujiza wa Roho Mtakatifu. Kuwaonyesha wale
wa1ioupokea ubatizo huo. Kuonyesha kusudi la
Ubatizo wa
aina hii.
C. Kwa
sababu wasiwasi na mashaka mengi yametokea katika jambo hilo, ni muhimu hasa
tulizungumze swali hilo na kuyapeleleza Maandiko ili tupate ukweli katika jambo
hilo.
I. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU:
A. Ile "ahadi" ya Yohana, Mt. 3:11.
B.
Ile "ahadi" ya Kristo,
Lk.
24:48-49.
1.
Iliwabidi "kungoja" katika mji wa Yerusalemu.
2.
Iliwabidi kupokea "uwezo"
utokao juu.
3.
Iliwabidi "kushuhudia".
C.
"Agizo" limetolewa mara ya pili, Mdo. 1:2-4.
D. "Uwezo" umeto1ewa mara ya pili, Mdo.
1:5.
Maangalizi:
1.
Kama huwezi kuyakinia kuhusu neno lile la Yohana katika Mt.
3: 11, ni nani anayesemwa, Yesu kwa
"kusema maneno yake tena"
na kwa "kuyaeeza" mbele ya Mitume, aeleza wazi kwamba ndio
"Mitume tu"
wanaohusika.
2.
Wale waliopokea ahadi ile, waliupokea "uwezo"
vile vile. Nani
walioupokea "uwezo"?
Mdo. 2:1-4, yaonyesha kwamba ni Mitume "tu" walioupokea
"uwezo" wa kusema kwa "lugha", 2:13.
Petro na wale kumi
na mmoja wengine, 2:14.
Pia fikiria neno
lile "wao" katika Mdo.
2:1 na Mdo. 1:26. Ni wazi kwamba ndioMitume wa1iohusika.
3.
Tangu wakati u1e tu Mitume "wa1ipoweka mikono yao" juu
ya mtu,
tunazo habari kwamba Mitume waliitenda
miujiza, 2:43; 3:3; 3:6; 4:33;
5:12; 5:15-16; 6:6,
8.
4.
Mitume wa1ikuwa mashahidi wa
pekee, Mdo. 1:22, pia
Mdo. 1:26 "akahehsabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja"; "sisi sote tu
mashahidi wake", Mdo. 2:32; wasikilizaji waliwasihi Mitume
walipowau1iza "watendeje",
Mdo. 2:37. Hiyo ndiyo itimilizayo amri ya
Yesu ya kusema, "ngojeni", "pokeeni uwezo",
"shuhudieni".
II.
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU ULITOKA MBINGUNI,
NILIKUWA WA
KUONEKA NA WA KISIKILIKA :
A. Ubatizo waRoho
Mtakatifu ulitoka mbinguni hasa,
ukakabidhiwa kwa
utumi
wa binadamu.
1.
"Mungu amekimwaga kitu hiki".
2. "Mnaehokiona sasa".
3.
Na "kukisikia,” Mdo. 2:33.
Maangalizi:
1.
Yalikuwa mafafanusi ya1iyosikilika, 2:2. Kitu fulani kilioneka; kwa hiyo ya1ikuwa mafafanusi ya1iyooneka, 2:3.
Kitu
fulani kilitendeka; walianza kusema kwa kwa
1ugha (lugha, Mdo. 2:7-12; "lugha zetu
wenyewe").
2. Hii siyo yale mathubutu yaliyo dhahiri katika "ahadi" ile ya Mdo. 2:39.
Yale
"ya1iyoahidiwa" na Yohana
na Yesu, yakapokelewa na
Mitume, siyo yale "yaliyoahidiwa kwa waamini wote. Siyo wote waliokuwa na kipawa cha lugha, 1 Kor.
12:10; 12:30, kwa hiyo "ahadi" mbili tofauti zahusika, 1
Kor. 12:29-31.
3.
Wote "waliobatizwa katika Roho
Mtakatifu" ndio wale
waliosema kwa lugha,
Mdo. 2:1-4; 2:6; 2:8; 2:11; 10:44-47. Laldni kulikuwa na wengine waliosema kwa kwa 1ugha
bila kubatizwa katika Roho,
Mdo. 19:1-6;
1 Kor. 12. Kwa
hiyo Mdo.
2:39 hauhusu Ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa
sababu, kama ingekuwa
hivyo, basi wote wangesema kwa lugha; lakini
Paulo akisema, "Je, wote wananena kwa
lugha?", anaonyesha wazi
kwamba sio wote. Lakini wote wameahidiwa kipawa cha Roho Mtakatifu;
kwa hiyo ni wazi kwamba ahadi ya Roho Mtakatifu haifuniki Ubatizo wa Roho Mtakatifu wala kipawa cha
lugha.
B.
Ubatizo wa
Roho Mtakatifu ulikuwa "ahadi", siyo amri.
C.
Ubatizo wa
Roho Mtakatifu ulifuatana na miujiza na
upuzio.
D. Ubatizo wa
Roho Mtakatifu haukukusudia ondoleo la dhambi wala kumweka mtu katika Kristo.
III.
KORNELIO NA NYUMBA YAKE WALIBATIZWA KATIKA ROHO
MTAKATIFU:
A. Kornelio "alibatizwa katika Roho
Mtakatifu", Mdo. 11:15-16.
B.
Hii iliitwa "karama ile ile", Mdo. 11:17, lakini hii ilikuwa tofauti na yote, isipokuwa yaliyotokea "mwanzo", 11:15, na juu
"yetu"
(yaani "Mitume tu.").
Maangalizi :
Ni wazi kwamba hiyo "karama ile ile "haikuwa kile "kipawa cha Roho
Mtakatifu" ambacho waamini wote
wameahidiwa; kama ingekuwa hivyo, Je ingaliandikwa kwa urefu wa
namna ile?
C.
Ubatizo wa
Kornelio katika Roho
Mtakatifu ulitangulia wongofu wake,
kwa hiyo ulikuwa kabla hajapokea ondoleo
la
dhambi, Mdo. 10:44.
Sasa soma Mdo.
11:4, "kwa taratibu," 11:15, Roho Mtakatifu alitangulia kabla ya imani, toba
au ubatizo! Lakini "kipawa cha Roho Mtakatifu" hufuata baada ya ubatizo kwa ondoleo
la
dhambi.
Maangalizi:
1.
Kupokelewa kwa
Roho Mtakatifu juu
ya nyumba ya Kornelio hakukuonyesha kwamba yeye amekwisha kuwa mtoto wa
Mungu.
2.
Neno lile "kipawa"
linaweza kuwa na maana mbalimbali tofauti kufuatana na mistari iliyopo. Mfano: Gal. 1:1
na Fil. 2:25 (Mitume). Katika mstari wa kwanza, ni mmoja wa wale kumi na
wawili; katika
mstari wa pili, ni "mmoja aliyetumwa na usharika".
D. Baada ya kupokea
ile karama ya mwujiza ya Roho
Mtakatifu, Kornelio na nyumba yake waIiagizwa wabatizwe, Mdo. 10:48; kwa
ondoleo la dhahmbi, Mdo.
2:38; wapokee kipawa
cha Roho Mtakatifu, Mdo. 2:38-39.
E. Kwa nini nyumba ya Kornelio waliupokea Ubatizo wa
Roho Mtakatifu?
1.
IIi ionyeshwe kwamba Mungu alikuwa amepokea,
mataifa vile vile na
Wayahudi, Mdo. 11:17-18.
2. IIi kanisa la Kristo liunganishwe, Mdo. 11:19-26.
Maangalizi:
Mungu alikuwa akingoja kwa
muda wa miaka kama kumi, mpaka aliwaita watu wake
kuwa Wakristo. Alifanya .hivyo tu,
baada Wayahudi walikuwa
wameyatambua mataifa kuwa
warithi wa uzima pamoja nao, na baada Wayahudi na mataifa walikuwa
wakisali pamoja katika usharika mmoja.
AZIMIO:
Ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa maonyesho ya Mungu ya kushangaza na yenye mwujiza! Ulikuwa mwanzo wa wakati mmoja maalum katika Ufalme wa Mungu,
na kwa hiyo ndio
wenye maana kwa watu
wa Mungu.
Matokeo yake yanaonekana hata leo,
lakini hakuna mtu leo awezaye kujinenakuwa na uwezo,
mathibitisho, na
maonyesho ya
aina hii. Lakini mtoto wa
Mungu mpaka leo hupata kipawa cha
"kuenea pote"
cha Roho Mtakatifu.
KIPAWA CHA KUENEA POTE CHA ROHO MTAKATIFU
INGIZO:
A. "Kipawa cha
Roho Mtakatifu" ni Roho
Mtakatifu mwenyewe anayetolewa kwa kila
mtu a1iyebatizwa akiwa mwamini atubuye.
B. Kuonyesha kwamba kipawa cha Roho Mtakatifu ni Roho
Mtakatifu mwenyewe, tena ni
kipawa cha kuenea pote
kwa watoto wa
Mungu.
C.
Roho Mtakatifu ameahidiwa kwa njia ya lIpuzio kwa watoto wote wa
Mungu; kwa hiyo aweza kuitwa "kipawa cha
kuenea pote".
I. "KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU"
KATIKA Mdo. 2:38
NI NINI?
A. "Kipawa ndicho Roho Mtakatifu (jinsi ya kujulisha mwenyewe)" A.
T. Robertson, Word Pictures of Greek
New
Testament.
B.
"Jinsi ya kujulisha kitu", N. Turner, Grammar of
New Testament Greek.
Kipawa kilikuwa Roho
Mtakatifu.
C.
Mara nyingi Mungu hayasemi yale ambayo "mimi" nataka ayaseme, lakini hata
hivyo nina wajibu
wa kujifunza na kuyapokea yale aliyoyasema.
II.
AHADI
ILIKUWA YA KUENEA POTE:
A."Ahadi ni kwa
ajili ya Wayahudi, na kwa
watoto wao, na kwa wote walio
mbali, na
kwa wote watakaoitwa na
Mungu." Mdo. 2:39. Kwa hiyo, kwa ajili ya Wayahudi na
mataifa - kwa
watu
wote,
ling. Efe. 2:11-13
(na mengine).
B.
Wote "walioitwa". Mungu
aitaje? Mdo. 2:37 "wakachomwa mioyo yao,” Mdo.
2:38 wafanye nini, Mdo.
2:40 wamc:onywa kufanya hivyo, Mdo.
2:41 waliolipokea
neno lake wakabatizwa, Mdo. 2:47
"wakiokolewa";
kwa hiyo wote walioyapokea masharti, wameahidiwa Roho. Wakati wote wanadamu waweza kusikia injili na
kuitii, Mungu ataitimiza ahadi yake ya kipawa
cha Roho Mtakatifu.
III.
WOKOVU -
JE,
HUO NDIO KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU?
A. SIYO! Hakusema, "tubuni mkabatizwe kwa ondoleo la
dhambi mtaokolewa."
Wokovu limo ndani ya ondoleo la dhambi. Ni lingine lililoahidiwa. Ni nini?
B.
Roho Mtakatifu mwenyewe!
IV. NENO -
JE,
HILO NDILO KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU?
SIYO!
Sababu "neno" halie1ezwi hivyo. Walilipokea neno
kabla hawajabatizwa,
kwa sababu walikuwa
"wamekatwa". "Maneno" yaliwaambia wafanye nini. Wote
walioyatenda walilipokea. "neno"; hata hivyo bade
kitu kingine kilielezwa. Neno
na roho siyo kitu kimoja. "Kipawa" kilikuwa kimeahidiwa, wakati waliokuwa wamekwisha pokea neno
na kubatizwa; kwa hiyo kile' "kipawa" siyo "neno la Mungu .. " Efe. 6:17.
V. MISTARI MINGINE IHUSUYO WAKRISTO WAKIPOKEA KIPAWA CHA
ROHO MTAKATIFU:
A. Mdo. 5:32,
mstari huu wasema kwamba Roho Mtakatifu hutolewa kwa
wale
watiio. Roho Mtalcatifu alikuwa ameahidiwa kwa
wale
waitiio injili, Mdo. 2:38.
Watiio watajwa
katika mistari yote miwili; jinsi gani twaweza lcuepuka, tusidhani
kwamba Roho
Mtalcatifu mwenyewe ametajwa katika mistari hiyo miwili?
B.
Mdo. 6:3, watu
hawa walikuwa "wenye kujawa
na Roho Mtakatifu". Bila shaka, hao
ndio wale wale wa Mdo.
2:38 na 5:32. Lakini, hata kama ikawa
hivyo walikuwa
tofauti na wale
wanafunzi wengine kwa aina fulani.
Sababu wote walikuwa na kile kipawa, bila shaka walikuwa
wamejitolea maisha
yao kwa
Roho na kwa Mungu, zidi kuliko
wengine walifanya. Miujiza haihusiki wala haitajwi hapo.
C. Rum. 8,
Roho, Roho wa Mungu, na Roho wa Kristo
hukaa ndani ya Wakristo, Rum. 8:9.
Katika 8:11, neno lile "kukaa" latoka kwa neno "nyumba au makao".
Neno hila halihusiki na
mahali pa
kusimamia kwa
mud
a tu, bali lahusika na
mahali pa kuishia
kwa kudumu. Lahusika na
kukaa kwa kudumu. Roho Mtakatifu
siyo mgeni wa siku moja tu, bali ni mkazi wa kudumu.
1.
"Anakaa" ndani yako hasa. Nini inayoufanya mstari huo
kuwa
kama
mfano?
2. Hautaji wala
hauhusiki na mfano wa kitu
kingine. "Kila neno
linenwalo, lazima lifahamike kufuatana na maana yake ya kawaida, isipokuwa jambo Ienyewe linenwalo au maneno mengine yanayotangulia na kufuata yanaikataza kwa jinsi maalum. Sheria hii yahusu maneno yote,
tena ni sheria
iliyo lazima." J.
D. Bales, The Holy
Spirit and Christians, uk. 10.
D. Gal. 4:4-6,
siyo kwa
maoni yetu wala Kwa upuzio,
bali ni kwa Roho kwamba twalia, "Aba,
yaani, Baba"" Roho yupi anakaa ndani yetu? Kwa hiyo tunaye
shahidi (Rum. 8:16) pamoja na
roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa
Mungu.
E. 1 Kor. 6:19-20,
Paulo adhihirisha, kwa nini Wakristo wasitende uasherati.
Paulo asema juu
ya
mwili wa mwanadamu uonekanao. Mwili huo
ndio hekalu la Mungu,
ambalo Mungu anakaa ndani yake kwa
Roho Mtakatifu. Asema wazi juu
ya "Roho
aliye ndani yenu". Labda hiyo ndiyo sababu kwamba kanisa au mwili
wa Kristo huitwa
hekalu la Roho Mtakatifu, 1 Kor.
3:16.
Maangalizi:
1. Mistari hii yaonyesha wazi kabisa kwamba Roho
Mtakatifu akaa ndani ya watu
wa Mungu.
2.
Anakaa ndani ya mtu zaidi ya mmoja, wakati ule ule.
3.
Tena hakuna lolote lililo kinyume cha akili, uwezekano,
au maandiko, kuhusu kukaa kwa
Roho Mtakatifu ndani ya mwili wa kibinadamu.
VI. ROHO MTAKATIFU AKIKAA "NDANI
YA
NENO TU":
A. Kuna ndugu wanyofu wengi wenye akili waammlO kwamba Roho
Mtakatifu anakaa ndani ya Wakristo kwa
njia
ya neno
tu. Lakini sisi hatuamini hayo. Ndugu hao waingia matatizo magumu ambayo hawawezi kuyashinda kwa
akili wala kwa maandiko.
1. Hakuna mstari hata mmoja usemao kwamba hivyo ndivyo Roho
Mtakatifu akaavyo ndani yetu.
2.
Hakuna mstari hata mmoja usemao kwamba Kristo
na Mungu wakaa ndani yetu kwa
njia ya neno
tu,
Efe. 2:22.
3.
Kupokelewa kwa
Roho Mtakatifu (ahadi yake katika Mdo.
2:38)
kulikuwa
baada ya kulisikia na kulitii neno.
4.
Tumetiwa muhuri na
Roho Mtakatifu katika Kristo, Efe. 1:13,
lakini
kwanza mmebatizwa katika Kristo, Gal. 3:27.
B.
Kwa
hiyo tumefahamu ya kwamba Roho Mtakatifu anakaa
ndani ya Mkristo
binafsi, na siyo kwa maneno ya Roho tu,
wakati maneno hayo yakipokelewa.
VII. ROHO MTAKATIFU ATAKAA NDANI
YA
MKRISTO KWA MUDA GANI?
A. Lini na kwa sababu
gani Roho Mtakatifu anamwacha mtoto wa
Mungu? Swali
hilo ni lile lile Ia kuuliza, Iini yule mtoto wa
Mungu anaanguka katika neema
asiirudie tena?
B.
Kanisa la Korintho lilikuwa usharika uliokuwa na ukosefu
wa dhambi nyingi; hata hivyo kanisa
lilikuwa hekalu la Roho Mtakatifu, 1 Kor.
3:16; na washarika hawakuwa mali yao wenyewe, maana "Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu". 1
Kor. 6:19.
C.
Roho Mtakatifu hatafuti udhuru
wa kutuacha, bali anahamu kubwa
ya kuwa
msaidizi wetu. Hata hivyo kuanguka kabisa huweza kutokea, na hutokea mara
nyingi, Ebr. 6:6; 10:26-31. Mkristo aweza kujifanya moyo wake
mgumu kiasi hiki
asiweze kumrudia Mungu tena. Wajibu wetu ni wazi. Kuishi maisha yetu kwa
ajili ya Mungu.
D. Wakati wote
ambao tunajaribu
na kuendelea mbe1e zaidi, tusiogope. Roho hatatuacha; lakini mara moja akituacha,
tutakuwa tumekufa kiroho mile1e.
Yakobo aliyaeleza hayo kwa mfano wa
kimwili, ili afundishe somo la
kiroho. "Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa." Yak. 2:26.
AZIMIO:
Kati ya faida na
wajibu ambazo Mkristo anazifurahia, kipawa cha
Roho Mtakatifu ndicho
cha muhimu sana.
lIe
ahadi iliyotolewa na
watu
waliotiwa pumzi ya Mungu wakati wa
mahubiri ya kwanza ya injili, yaonyesha jinsi Mungu aonavyo juu
ya
Roho akikaa ndani ya Mkristo. Mungu
atusaidie tuweke hazina ya jambo hila ili tujitahidi kuishi maisha yetu
kufuatana na hayo.